Mwenyekiti wa taifa wa chama cha demokrasia
na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe
amewaagiza madiwani wa halmashauri ya
manispaa ya Bukoba wanaotokana na vyama
vinavyounda umoja wa katiba (UKAWA) ambao
unaongoza manispaa hiyo kuhakikisha
wanawashirikisha wananchi katika kila hatua
inayofikiwa inayohusiana na mchakato mzima wa
mradi wa ujenzi wa soko kuu jipya la Bukoba.
Ametoa agizo hilo baada ya kutembelea soko la
sasa la mji wa Bukoba ambalo ujenzi wake
ulikwama kutokana na migogoro iliyojitokeza
miongoni mwa madiwani wa manispaa hiyo
ambao ulipekelekea baadhi ya madiwani
kugomea vikao kwa zaidi ya miaka miwili jambo
lililopelekea baadhi yao kuvuliwa nyazifa zao za
udiwani kwa amri ya mahakama, Mbowe
amesema kuwashirikisha wananchi katika
utekelezwaji wa miradi wa soko kuu la Bukoba ni
namna ya kuweka mambo wazi jambo
linalopunguza migogoro isiyo na tija ndani ya
jamii.
Nao, baadhi ya wafanyabiashara katika soko hilo
wameunga mkono kauli iliyotolewa na mwenyekiti
huyo ya suala la kuwashirikisha wananchi,
wakizungumza kwa nyakati tofauti wameeleza
kuwa hawakupinga mradi wa ujenzi wa soko kuu
la Bukoba uliokwama bali walichokitaka ni uwazi
na pia walitaka kuonyeshwa maeneo mbadala
ambayo wangeyatumia kufanya shughuli zao za
kibiashara baada ya kupisha mradi wa ujenzi wa
soko hilo, hivyo wamesema mradi huo ukiwa wazi
wataupokea.
Kwa upande wake, mbunge wa jimbo la Bukoba
mjini, Wilfred Lwakatare akizungumza amesema
mipango madhubuti ya kuufufua mradi wa ujenzi
wa soko jipya la Bukoba imeishafanyika na
mchakato wa kuwatafutia maeneo mbadala
wafanyabiashara katika soko hilo unaendelea na
umeishafikia katika hatua nzuri.
Uncategories
Madiwani wa UKAWA waagizwa
kuwashirikisha wananchi katika ujenzi wa
soko kuu la Bukoba.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon