Wakati baadhi ya vyama vya siasa vimetangaza
kujitoa uchaguzi wa marudio Zanzibar, tume ya
uchaguzi -ZEC- imetoa msimamao wake na
kusema wagombea wote ni halali na watagombea
nafasi zao kwa vile hakuna hata chama kimoja
kilichofuata sheria na kanuni za uchaguzi.
Msimaamo huo wa tume umetolewa na
mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi ya
Zanzibar Jecha Salum Jecha katika taarifa yake
kwa vyombo vya habari ambapo amesema kuna
utaratibu wakujitoa na kwa mujibu wa sheria na
kanuni za uchaguzi hakuna chama kilichofuata
kanuni ikiwa ni pamoja na wadhamini
wawagombea kutangaza kuondoa udhamini wao,
hivyo wagombea wote wa urais, uwakilshi na
udiwani wote bado ni halali.
Akizungumzia maandalizi hayo amesema
yanaenda vizuri ikiwa ni pamoja na uteuzi wa
wasimamizi wa uchaguzi, upangaji wa vifaa,
mawasilaino na vyama na uchapishaji wa dafatri
na mafunzo na wagombea kuanza kupatiwa ulinzi
na haki zote kwa mujibu washeria huku akielzea
karatasi za kura amabzo zinachapwa nje
zinatarajiwa kuwasili mapema mwezi ujao.
Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi vyama
amabvyo vimethibitisha kushiriki ni pamoja na
CCM, TADEA, ADC, CCK, AFP, SAU, TLP, huku
CUF, NRA, CHAUMA, DP, Jahazi asilia na ACT
Wazalendo ambao mgombea wake Khamis Lilla
ametangaza kugombea huku chama chake
kikimufukuza uanachama.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon