Kituo kipya cha afya cha Mwendakulima
kilichoko wilayani Kahama katika mkoa wa
Shinyanga kinakabiliwa na changamoto kubwa ya
ukosefu wa dawa, vifaatiba pamoja na uhaba wa
wahudumu hali ambayo inasababisha wananchi
wanaoishi katika kijiji hicho kufuata huduma za
kiafya katika vituo vilivyoko katika vijiji vya jirani
wakihofia kutopata huduma bora katika kituo
hicho cha afya cha Mwendakulima.
Akizungumzia changamoto zinazokikabili kituo
cha afya cha Mwendakulima ambacho
kimejengwa kwa ufadhili wa kampuni ya ACACIA
inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Buzwagi
muuguzi mfawidhi katika kituo hicho Bi.Selestina
mbezi ameiomba serikali kupeleka wahudumu wa
afya katika kituo hicho pamoja na kukipatia dawa
na vifaa tiba vya kutosha ili kuokoa maisha ya
wananchi wanaotumia muda mrefu kufuata
huduma za kiafya katika vituo vingine vilivyoko
mbali na kijiji hicho hali inayotishia kupoteza
maisha ya wagonjwa hususan wanawake
wajawazito.
Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya
Mwendakulima Bw.Mussa Ibingo amedai kuwa
serikali inatambua mchango wa kampuni ya
ACACIA katika kufadhili miradi mbalimbali ya
maendeleo ya jamii hivyo kuna kila sababu za
kuhakikisha serikali inapeleka dawa na vifaatiba
vya kutosha katika kituo hicho mapema
iwezekanavyo huku baadhi ya wagonjwa
waliokuwa wakitibiwa katika kituo hicho cha afya
wakionyesha kuridhishwa na kuduma waliyoipata.
Uncategories
Kahama:Kituo cha afya cha Mwendakulima
kinakabiliwa na upungufu wa dawa na vifaa
tiba Shinyanga.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon