BALOZI SIMBA AWAPONGEZA WAOKOAJI AJALI YA MV KILOMBERO

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati)
pamoja na ujumbe wake, wakiingia katika lango
kuu la kuingilia abiria wakati alipotembelea
eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero II na
kushuhudia shughuli za uokoaji wa magari,
utafutaji miili ya watu na uokoaji wa kivuko
hicho ukiendelea. Balozi Simba alifanya ziara ya
kikazi mkoani Morogoro kwa kutembelea miradi
ya maendeleo ya Jeshi la Magereza mkoani
humo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia),
akisalimiana na Askari wa Kikosi cha Wanamaji
wa Uokoaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao
wanashiriki katika shughuli za uokoaji miili ya
watu waliozama baada ya kivuko cha MV
Kilombero II kuzama Januari 27.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akiongozana
na ujumbe wake kuelekea eneo la tukio ambapo
kivuko cha MV Kilombero II kilizama wiki
iliyopita. Kulia ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma
Malewa. Katikati ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Morogoro, SACP Dkt. Kato Lugainunura.
Katibu Tawala Wilaya ya Kilombero, Yahya
Naniya (kulia), akitoa maelezo juu ya shughuli
za uokoaji zinavyoendelea kwa Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Balozi Simba Yahya (wa tatu kushoto) na ujumbe
aliofuatana nao mara baada ya kufika eneo
kilipozama kivuko cha MV Kilombero II wiki
iliyopita. Naibu Katibu Mkuu alikuwa mkoani
Morogoro mwishoni mwa wiki kwa ziara ya
kikazi.
Wasamaria wema waliojitolea kushiriki zoezi la
uokoaji katika ajali ya kivuko cha MV Kilombero
II kilichotokea wiki iliyopita mkoani Morogoro,
wakimuelekeza dereva wa gari la kunyanyua vitu
vizito (halipo pichani), wakati wa uokoaji wa
moja ya magari yaliyozama wakati wa ajali hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) na
ujumbe aliofuatana nao wakiangalia shughuli za
uokoaji zinavyoendelea mara baada ya kivuko
cha MV Kilombero kuzama huku baadhi ya vitu
vikiokolewa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akiondoka
eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero mara
baada ya kushuhudia shughuli za uokoaji
zikiendelea vizuri.
(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi).

Previous
Next Post »

Ads Inside Post