Familia kadhaa hazina mahali pa kuishi katika
kata ya Serera wilaya ya Monduli baada ya moto
kutelekeza nyumba walizokuwa wanaishi pamoja
na maduka makubwa nane ya jumla hoteli na bar
na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha
kwa wathirika wa tukio ilo.
Wakizungumza katika eneo la tukio mashuhuda
na waathirika wa moto wamesema tukio ilo
lilianza majira ya saa kumi na moja alfajiri na
kwamba wamejitahidi kuuzima lakini juhudi
zilishindikana kutoka na kukosa vifaa vya kuzima
moto hivyo hakuna kilicho salimika na wengi wao
wanadaiwa katika taasisi za fedha huku taarifa
zisizo thibitishwa zinadai kuwa moto huo
ulishababishwa na itilafu ya umeme.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli Isack
Joseph amesema tukio ilo ni la pili kutokea
wilaya humo katika kipindi kisicho zidi wiki mbili
hivyo serikali inapaswa kuchunguza chanzo na
kudhibiti ili kupunguza madhara wanayo yapata
wananchi.
Akizungumza akiwa katika eneo la tukio mkuu wa
wilaya ya Monduli Francis Miti amesema wilaya
hiyo inakabiliwa na ukosefu wa magari ya
zimamoto kwani inategemea gari moja tu ambalo
ni la uwanja wa ndege wa manyara na hata hivyo
gari ilo kwa sasa limeharibika
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon