Kufungwa Kwa Simu Bandia Wananchi na wafanyabiashara wapaza sauti

Sekta ya mawasiliano ni miongoni mwa
sekta zinazokuwa kwa kasi nchini Tanzania,
ikiwa inatajwa kuchangia kwa wastani mzuri
katika pato la taifa.
Ukuaji huo unakwenda sambamba na
uingizwaji wa vifaa na teknolojia mbalimbali
hususani simu za mkononi kwa mtumiaji wa
mawasiliano na mlaji wa habari.
Azma ya Serikali ifikapo Juni 17, 2016 ni
kuzifungia simu zote bandia zilizopo nchini
ili kukidhi ukuaji wa sekta hiyo na kudhibiti
mianya ya uhalifu kupitia simu zisizokidhi
viwango.
Zaidi ya kadi za simu milioni 30 zinamilikiwa
na watanzania idadi hiyo iki akisi zaidi ya
simu za mkononi milioni kumi na tano hii ni
kutokana na takwimu za mamlaka ya
mawasilino ya Tanzania TCRA mwaka 2015.
Serikali imetangaza kuzifunga simu bandia
ifikapo Juni /17 /2016 hii nikutokana na
hatari ya matumuizi ya bidhaa sanjari na
kuthibiti ubora wa bidhaa zinazoingia na
kutumiwa nchini.
Utafiti uliofanywa na star tv katika jijini
Mwanza katika wilaya za Nyamagana(map
of Mwanza area shot ) na Ilemela
umebainisha ufahamu mdogo wa wananchi
juu ya hatua hiyo lakini pia umeonyesha
kuwa idadi kubwa hawawezi kutofautisha
simu bandia na yenye kukidhi viwango kama
jedwali linavyofafanua.
Kifungu cha 84 cha sheria ya mawasiliano
ya kielekitroniki na posta EPOCA 2010
kinataka kuwepo kwa mfumo unaotambua
namba za utambulisho wa vifaa vya
mawasiliano ya mkononi. Utekelezaji wa
azimio la serikali katika kudhibiti matumizi
ya simu za mkononi zisizokidhi viwango
huenda likafungua sura mpya katika
kuwajengea wananchi utamaduni wa
kununua na kutumia bidhaa zilizothibitishwa
ubora na mamlaka husika.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post