Makamu Mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni Rais wa
Zanzibar Dokta Ali Mohammed Shein
ametaka wananchi na wanasiasa kuendelea
kutunza na kuhubiri amani wakati wa
kuelekea uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Amesema kuwa amani ni kitu pekee
kitakachoivusha Zanzibar na changamoto
zilizopo za kisiasa akisisitiza kuwa si vyema
kushabikia baadhi ya vyombo vya habari na
mitandao ya kijamii inayopotosha ukweli
uliopo.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa
sherehe za kutimia miaka 39 tangu kuzaliwa
kwa chama cha mapinduzi 5/2 /1977 katia
kiwanja cha Amaan mjini Zanzibar.
Dr.Shein ametumia fursa hiyo kuwataka
wanaccm kujipanga katika kuimarisha
chama .ila suala la kurejea uchaguzi halina
mbadala ila suala la amani ya nchi ni
mwanzo na hatokubali kuona inachezewa.
Nae katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi
Taifa Abrahman Kinana amesema CCM
imejipanga vyema kurejea uchaguzi kwa
mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa na
na TUME YA UCHAGUZI Kwa kutambuwa
uchaguzi ni mahesabu na mikakati
wamejiandaa vyema.
Kuhusiana na maneno yanayosambazwa
katika mitandao na baadhi ya watu
yanayoashiria fujo ama vitisho katika kipindi
cha uchaguzi Mjumbe wa kamati kuu
ambae pia ni Makamu wa pili wa Rais wa
anzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema kuwa
serikali imejipanga kulinda amani kwa hali
yeyote ,huku akiwashauri vijana kutokubali
kushawishiwa na kujiingizakatika vitendo
vya uvunjifu wa amani ili kujiepusha na
matatizo.
Kilele cha sherehe za miaka 39 ya CCM
kinatarajiwa kufanyika Mkoani Singida
mnamo tarehe 6 Febuary Mgeni rasmi
akitegemewa kuwa ni Mwenyekiti CCM Taifa
Dr Jakaya Mrisho Kikwete.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon