Ikiwa imepita siku moja toka mbunge wa Geita
Vijijini, Joseph Msukuma (CCM), kusema haoni
sababu ya serikali kuzuia bangi kuwa zao la
biashara kwa maana haoni madhara yake huku
akidai kwamba viroba vina madhara zaidi kuliko
bangi, Afande Sele amefunguka na kusema
serikali ihalalishe matumizi ya bangi na si
kukosoa juu ya hoja hiyo ya Joseph Msukuma.
Afande Sele amedai kuwa kuna nchi ambazo
tayari wao wamehalalisha matumizi ya bangi na
kuthibitisha kuwa pombe ina madhara makubwa
zaidi kuliko bangi.
"Legalize it, Don't criticize it. Korea, Kaskazini,
Marekani, Mexico Uruguay na mataifa mengine
ya Ulaya yamethibitisha pombe ina madhara
kuliko Cannabis Sativa" Alisema Afande Sele.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon