Jaji Lubuva abaniisha mipaka ya Rais kwa tume ya uchaguzi

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini
Tanzania, Jaji Damian Lubuva amebainisha
wazi kuwa rais wa jamuhuri ya muungano
wa Tanzania hana mamlaka yeyote juu ya
maamuzi ya yanayofanywa na tume ya
uchaguzi.
Kumekuwepo na shinikizo la kumtaka Rais
Magufuli kungilia maamuzi ya tume ya
uchaguzi ya Zanzibar jambo ambalo
limetajwa kuwa nikinyume na sheria,kanuni
na taratibu za tume ya uchaguzi.
Lubuva ameyasema hayo baada ya kufanya
kikao na Rais John Pombe Magufuli
alipomtembelea Ikulu, jijini Dar es Salaam
Kauli ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi
nchini, Damian Lubuva imekuwa wazi hapa
kuhusu iwapo Rais au kiongozi yoyote Yule,
anapaswa kujihusisha na maamuzi
yanayotekelezwa na tume hiyo.
Ameyasema hayo licha ya madai kuwa Rais
ameshindwa kuleta mwafaka kuhusu
kufutiliwa kwa uchaguzi wa Zanzibar katika
uchaguzi uliopita.
Lubuva amesisitiza kuwa tume hiyo ni huru
na haijawahi kuingiliwa kimaamuzi na
kiongozi yoyote.
Huku hali ya hati hati ikiendelea kukumba
mchakato wa marudio ya uchaguzi wa
Zanzibar tume hiyo inajivunia mamlaka
kikatiba ya kuwa na msimamo dhabiti
ambao kisheria haupaswi kuingiliwa kwa
lengo la kubadilishwa na kiongozi yoyote
Ziara aliyoifanya ikulu jijini Dar es Salaam
ilikuwa ni ya kumtaarifu Rais juu ya
yaliyojiri katika kikao cha Jumuiya ya Afrika
Mashariki kilichofanyika Mjini Kampala,
Uganda na kujadili kuhusu uchaguzi Mkuu
wa Uganda unaotarajiwa kufanyika tarehe
18 mwezi huu.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post