Watanzania wamejigamba kufanya vyema
katika mbio za kimataifa za kilimanjaro
Marathon zinazotarajiwa kutimua vumbi
hapo Jumapili hi Feb katika viwanja vya
Ushirika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Tayari maandalizi ya Mbio hizo
yamekamilika huku zaidi ya washiriki elfu 8
kutoka mataifa 45Duniani kote wakitarajiwa
kushiriki mbio hizo.
Ikiwa ni miaka kumi na nne sasa tangu
kuanzishwa kwa mbio za Kilimarathoni,
Mwaka huu masindano hayo yanaonekana
kuwa na muamko mkubwa zaidi huku watu
kutoka mataifa mbalimbali wakijitokeza kwa
wingi kujiandikisha tayari kushiriki mbio hizo
siku ya kesho.
Safari hii watanzania wamejigamba
kuwabwaga wanariadha kutoka Kenya
ambao wamekuwa wakitawala mbio ndefu
za km 42 huku watanzania wakibaki kuwa
wasindikizaji.
Hata hivyo Wadhamini wa mbio hizo mwaka
huu Bia ya Kilimanjaro,Tigo pamoja na
Gapco wanajigamba kutoa donge nono kwa
washindi .
Mbio hizo za kimataifa zinatarajiwa
kuhudhuriwa na Waziri wa Habari,
utamaduni, sanaa na Michezo Nape
Nnauye.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon