Hali ya hatari imeibuka katika kijiji cha Kutishi
mpakani mwa wilaya za Kondoa na Simanjiro
baada ya watu wa jamii ya kifugaji kutoka
makabila ya Maasai na Watatoga wakiwa na silaa
za jadi mikuki mishale na silaa za moto zikiwemo
bunduki kutaka kupambana kwa madai ya
kuibiana Ng’ombe hali iliyo lilazimu jeshi la polisi
kuingika kati kutuliza ghasia hizo huku ikidaiwa
watu watatu Maasai wawili na Mtatoga
wamefarikiduni katika ugomvi huo.
ITV ilifika katika eneo ilo na kushuhudia watu hao
wa jamii ya kifugaji kutoka kabila la masai na
watatoga wakiwa na silaa mbalimbali za jadi na
bunduki wakiwa wamesimama tofati ya mita
miambili na jeshi la polisi likiwa katikati kuzuia
wasikaribiane huku kila Maasai wakidai
hawataondoka bila kupatiwa Ng’ombe wao na
Watatoga wakidai ndugu yao anayedaiwa kuuawa
ambapo viongozi wa mila wametumia nguvu
kubwa kutuliza ghasia hizo.
Katika tukio ilo viongozi wa mila kutoka jamii
hizo walitumia nguvu kubwa kuwatuliza vijana
walikuwa na jazba ambao walitaka kuvamiana
wakiwa katika eneo la Mbuga Tambalale katika
pori la akiba la Mkungunero.
Mbunge wa Simanjiiro James Ole Milya ameitaka
serikali kutopuuuzia hali hiyo kwakuwa
imeonesha kila dalili za uvuchifu wa amani na
hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwani kila dakika
zinavyo kwenda ndiyo watu wanavyo badilika.
Uncategories
Jeshi la polisi lazima ghasia kati ya
Wamasai na Watatoga mpakani mwa
Simanjiro na Kondoa.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon