Wizara ya mambo ya ndani kupitia jeshi la polisi
wameanzisha mpango maaalum wa kuhakisha
usalama wa raia na mali zao unaimarika ambapo
waziri Mh Charles Kitwanga amemwagiza mkuu
wa jeshi la polisi nchini Ernest Mangu
kuhakikisha kuwa mpango huo unatekeleza kama
ulivyopangwa lengo likiwa ni kuona matukio ya
kihalifu yanapungua kama siyo kuisha kabisa.
Mh Kitwanga ametoa agizo hilo muda mfupi
baada ya kusaini mkataba wa makubaliano baina
ya waziri Kitwanga na IGP Mangu kuwa jeshi la
polisi litatekeleza mpango huo ambao
unaratibiwa kupitia mradi wa matokeo makubwa
sasa.
Naye kamanda IGP amesema wamejipanga
vyema kuhakisha kuwa wanatekeleza mpango
huo na kwa kuanza wataanza na wilaya ya
Kinondoni kwa sababu ndio inayongoza kwa
matukio ya kihalifu.
Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa BRN
Bw Omari Isa amesema kabla ya kupatikana kwa
mpango huo maafisa wa polisi na viongozi
mbalimbali wa serikali za mitaa walikaa chini na
kukubaliana ni mambo gani ya msingi ambayo
watatakiwa kuyafanyia kazi na ni kwa namna
gani.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon