Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera yaendesha operation ya kuwanasa watumishi walevi.

Uongozi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa
kagera iliyoko katika manispaa ya bukoba
umeendesha operation maalumu iliyokuwa ya
kushtukiza kwa lengo la kuwasaka na kuwabaini
baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo ambao
hujihusisha na vitendo vya ulevi wakati wa muda
wa kazi badala ya kutoa huduma kwa wananchi.
Operation hiyo maalumu imeongozwa na katibu
wa hospitali hiyo ya rufaa, Kilwanila Kiiza na
imeendeshwa kwenye maeneo mbalimbali ya
vilabu vya pombe za kienyeji zilizoko maeneo ya
uswahilini na baadhi ya mabaa yaliyoko karibu na
hospitali hiyo, katika operation hiyo uongozi huo
umefanikiwa kuwanasa watumishi wawili wa
kitengo cha ufundi ambao ni pamoja na Salvatory
Rwegasira na Godfrey Mganyizi waliofanikiwa
kukimbia kabla ya kutiwa mbaroni, kwa pamoja
walikuwa wakinywa pombe za kienyeji aina ya
gongo.
Katibu huyo amesema hospitali itawachukulia
hatua za kinidhamu watumishi hao wawili ili iwe
wawe mfano kwa watumishi wengine ambao
wanajihusisha na vitendo vya kutoroka wakati wa
muda wa kazi na kwenda kwenye ulevi,
amesema uongozi wa hospitali hiyo umeendesha
operation hiyo maalumu kwa lengo la kijiridhisha
kufuatia taarifa zilizokuwa zikwasilishwa ofisini
kwake.
Kwa upande wake Amos Byabato mkuu wa
kitengo cha ufundi cha hospitali ya rufaa ya
mkoa wa kagera akizungumza amesema
watumishi hao mara kwa mara wamekuwa
wakiondoka kazini bila kuaga, ameleeza kuwa
wanapoingia kazini baada ya kusaini kitabu cha
mahudhurio kuwa huondoka bila kuaga na
kuelekea katika maeneo yasiyojulikana ambapo
wakati mwingine hurudi kesho yake.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post