Agizo la mkuu wa mkoa wa Mwanza la kupiga
marufuku magari yanayotoa huduma za usafiri
jijini humo ‘HIACE ‘ pamoja na Pikipiki za abiria
maarufu kama bodaboda, kufanya kazi wakati
zoezi la usafi wa mazingira likiwa linaendelea,
limegonga mwamba baada ya ITV kushuhudia
pikipiki na magari yakiendelea kusafirisha abiria
kama kawaida.
Agizo hilo lililotolewa januari 30 mwaka huu na
mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo,
mbele ya naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu
wa rais muungano na Mazingira Mh.Luhaga
Mpina limepuuzwa na madereva wa HIACE na
bodaboda jijini Mwanza.
Madereva hao wa vyombo vya moto wamenaswa
na kamera ya kituo hiki wakiendelea kusafirisha
abiria kama kawaida, huku kaimu mkuu wa mkoa
wa Mwanza Baraka Konisaga akishindwa
kuwachukulia hatua za kuwadhibiti.
ITV pia imeshuhudia baadhi ya askari wa kikosi
cha usalama barabarani katika eneo la Pepsi na
kituo cha polisi Pamba ambao waliagizwa
kuyakamata magari yote ya abiria na pikipiki na
kisha kuyatoza faini ya shilingi 30,000 kwa
kukaidi agizo la serikali,wakiishia kuyatazama tu
huku magari hayo yakisababisha usumbufu
mkubwa kwa wananchi waliokuwa wakifanya
usafi barabarani.
Hata hivyo zoezi la usafi katika maeneo
mbalimbali ya jiji la Mwanza limeoonekana
kudorora tofauti na siku zingine, huku baadhi ya
watanzania wenye asili ya kiasia wakihamasika
kwa wingi kufanya usafi katika mtaa wa
makoroboi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mwanza
Adam Mugoyi amewaonya watu wanaoendelea
kutupa ovyo takataka, huku mbunge wa jimbo la
nyamagana Mh.Stanslaus Mabula akikiri zoezi
hilo kukumbwa na changamoto ya vyombo vya
usafiri.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon