Kutoa mimba ni nini? Hii ni hali ya
mwanamke kwa hiari yake mwenyewe
kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi
chake.
Kutokana kuongezeka kwa idadi ya
mahusiano duniani na kutotumia njia za
uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko
kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa
sasa wanatoa mimba.
Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua
kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana
wanaokua kwenye mahusiano na wanaume
zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa
mimba na asilimia tano tu ya wote ndio
wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu
ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka
tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo
au mfu?
Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta
wamebeba mimba zingine wakati watoto
wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa.
Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa
aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika
lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa
mpango kama condomu kuzuia mimba na
kama kondomu huiwezi basi tumia njia
zingine kama sindano na vijiti kwasababu
wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu
isipokuepo ndio basi tena.
Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba
kama ifuatavyo…
Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland
mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake
wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa
mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi
mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa
na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa
maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya
kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo
ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba
hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya
dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye
mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya
uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba
moja uwezekano wa kufa unakua 45%,
mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.
Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake wengi
ambao wanalia kutopata watoto wana
historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na
wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa
maamuzi yao. Hii inatokana na madhara
makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa
uzazi baada ya mimba kutoka.
Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu
amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye
mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai
kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi.
Lakini utoaji wa mimba huambatana na
magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando
huo na kusababisha mimba kukulia
huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija
husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..
Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko
uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo
yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla
ya mda husika akibeba mimba nyingine.
Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla
ya muda maalumu na viungo ambavyo
havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua
wagonjwa wa akili maisha yao yote.
kansa ya mlango wa uzazi
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari
kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi
kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii
ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango
huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya
kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya
homoni za uzazi.
Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie
maamuzi yake ya kutoa mimba siku za
usoni hata kama hakupata madhara yeyote
hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani
maisha yake yote na itakua inamuumiza
usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu
ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia
wakati hayupo, kua na hasira sana…
Mwisho
kumbuka kila mwaka wanawake 70000
wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya
kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya
kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa
hivi unawaona malaya ipo siku
utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari
kwamba labda itokee miujiza ndo
utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za
uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa
mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto
ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha
yako yote..
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon