Sasa ni rasmi wimbo wa rapa Ney wa Mitego
‘shika adabu yako’, umefungiwa na Baraza la
sanaa Tanzania BASATA.
Taarifa rasmi kutoka BASATA inasema kuwa
mbali na kuufungia wimbo huo, itatoa onyo kali
kwa msanii huyo kuacha kutoa nyimbo zenye
maudhui ya kuudhi na kinyume cha maadili.
BASATA pia limemtaka msanii huyo kuacha
kuiongelea ‘ngoma’ hiyo katika vyombo vya
habari kwa namna yoyote ile
Usome waraka mzima wa BASATA na maamuzi
yao hapo chini,
Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 4
(1) (j) cha sheria ya BASATA
namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepwa
mamlaka ya kuratibu na kufuatilia
mienendo ya mtu yeyote anayehusika na kazi za
Sanaa na kuhakikisha
linalinda maadili ya kitaifa miongoni mwa
Wasanii wanapokuwa jukwaani au
wanapobuni kazi yoyote ya Sanaa.
Aidha, kifungu cha 4 (2) cha sheria hii kinalipa
Baraza nguvu ya
kisheria kufanya jambo lolote lile kuliwezesha
kufanya majukumu yake kwa
faida na ustawi wataifa.
Baraza la Sanaa la Taifa limekuwa likipokea
simu za maswali na
malalamiko kadhaa kutoka kwa waandishi wa
habari na wadau wa Sanaa ambao
kwa njia moja ama nyingine wameguswa na
kuchukizwa na kazi hiyo ambayo
si tu inadhalilisha tasnia ya Sanaa bali
inawafanya watu makini kuanza
kuhoji hadhi ya msanii, weledi na taaluma ya
Sanaa kwa ujumla.
BASATA mara kadhaa limekuwa likikemea na
kuchukua hatua kadhaa dhidi ya
tabia hii chafu ambayo ilianza kujitokeza
kwenye kampeni za uchaguzi
mkuu wa mwaka jana wa 2015. Kukemea huku
ni kwa msingi mmoja kwamba
asili ya tasnia hii ya Sanaa ni kuelimisha jamii,
kukosoa pale
kunapokuwa na tatizo, kuburudisha na kujenga
jamii yenye staha, umoja wa
kitaifa, mshikamano na amani.
Ni wazi wasanii wengi wanafanya kazi zao
vizuri, kwa kubuni kazi zenye
ubora, zenye kujenga jamii na zaidi
zinazoburudisha rika zote kiasi cha
kuzifanya zililetee heshima taifa. Kati ya hawa
wengi, kuna wachache
ambao wanaipaka matope tasnia ya Sanaa na
kwa kiasi kikubwa wanaonesha
wazi kutokuwa na nia njema.
Kwa mantiki hii BASATA halitavumilia hawa
‘wasanii’ wachache ambao
wanataka kuigeuza tasnia ya Sanaa na wasanii
genge la wahuni, wasio na
staha, wa kudharaulika na waliojipanga
kuibomoa jamii na kuharibu amani
na utulivu uliopo nchini.
BASATA linapenda kueleza yafuatayo:
1. Vyombo vya habari viwe vya kwanza kuchuja
maudhui ya kazi yoyote ya
Sanaa kabla ya kuingia kwenye mtego wa kuwa
mawakala wa uharibifu wa
jamii kupitia kucheza kazi chafu za Sanaa.
BASATA lilishaziandikia radio
zote kuzishauri kuwa na kamati za maudhui ya
kazi za Sanaa lakini
inashangaza baadhi ya vyombo vya habari
vinakuwa vya kwanza kushabikia
nyimbo hizo chafu na kuwapa muda mrefu wa
mahojiano wasanii hao na
baadaye kurudi BASATA kuhoji uhalali wa
nyimbo husika. Hii si sawa hata
kidogo.
2. Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.
John Pombe Magufuli
imejipanga kuwajengea mazingira bora ya
utendaji Wasanii wote nchini
kupitia kuboresha miundombinu ya Sera, Sheria
na Kanuni. Hata hivyo,
uwepo wa Wasanii kama hawa unafanya jamii
kuhoji hadhi ya wasanii,
nafasi yao katika jamii na kwa maana hiyo
kukatisha tamaa juhudi za
kuipa msukumo sekta hii maana wadau wakuu
ambao ni wasanii wanaanza
kuoneasha kuwa mawakala wa uharibifu wa
jamii.
3. BASATA linawataka wasanii kujiuliza mara
mbili kabla ya kubuni kazi
zao za Sanaa. Wafikirie wazazi, ndugu, jamaa na
marafiki zao
watazipokeaje? Wavae nafasi ya wale
wanaowatukana na kuwadhalilisha,
Waelewe kwamba Sanaa si uwanja wa kutusi na
kudhalilisha watu hata
kidogo. Ikitokea wale wanaotukanwa na
kudhalilishwa kughafilika Sanaa
itakuwa uwanja wa vita. Hili halikubaliki.
4. Tunafahamu kuna wasanii wamekuwa
wakifanya hivyo makusudi kutafuta
‘umaarufu uchwara’ ambao wanadhani utakuja
kutokana na kuzungumziwa
sana. Tunapenda kusema wazi kwamba
umaarufu hauji kwa upuuzi wa namna
hiyo unakuja kwa msanii mwenyewe
kujiheshimu, kujituma, kubuni kazi bora
na zenye kulifahamu vema soko la ndani na la
kimataifa.
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA
KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA
Uncategories
NI RASMI SASA BASATA
WAIFUNGIA ‘SHIKA ADABU YAKO’
YA NEY WA MITEGO, SABABU ZIPO
HAPA KWENYE HUU WARAKA WAO.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon