Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Geita
imewakamata raia 16 wa China ambao
wapo nchini wakifanya kazi katika maeneo
ya uchimbaji kinyume na taratibu.
Wachina hao ambao wameingia nchini kwa
nyakati tofauti, hati zao za kusafiria
zinaonyesha kuwa wamekuja kutalii lakini
wamejiingiza katika ajira kwenye mgodi wa
Eagle Brand Mining Investment
unaojihusisha na uchimbaji wa dhahabu
kwenye kijiji cha Nyamahuna.
Wachina hao wameingia kuanzia mwezi
novemba mwaka jana ambapo aliyewaleta bi
Rehema Abdallah Mmiliki Mgodi wa Eagle
Brand Mining Investment amedai kuwa
wamekuja kwa ajili ya kumfungia mashine.
Charle Washima Afisa Uhamiaji Mkoa wa
Geita amesema Wachina hao waliokamatwa
hawana vibali vya kufanya kazi na kuishi
nchini.
Baadhi ya wafanyakazi wanaofanya kazi
katika mgodi huo wamesema wachina hao
wapo katika kufanya shughuli mbalimbali
lakini imekuwa vigumu kupata ujuzi
kutokana na wachina kutojua kingereza
lakini pia kutowafundisha.
Afisa Uhamiaji Charles Washima alitumia
nafasi hiyo kuwataka wananchi wanapoona
wageni wasiowatambua ni vyema wakatoa
taarifa ili wafatiliwe kama wana uhalali wa
kuishi nchini.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon