Fursa katika Ujasiliamali wa Kiteknolojia

Ujasiariamali unahubiriwa kila kukicha, hasa
hapa nyumbani kwetu Afrika ambapo
upatikanaji wa kazi unazidi kuwa changamoto.
Moja ya sekta zinazotiliwa mkazo zaidi
kwenye mahubiri haya ni ujasiliamari
unaohusikia na teknolojia. Hii ni kwa sababu
teknolojia inakuwa kwa kasi ya kuridhisha
barani Afrika.
Picha Na the-star.co.ke
Viashiria vya Ujasiliamari -Teknolojia Kukuwa
Si muda mrefu sana tangu raisi Barack Obama
wa Marekani, kufungua mkutano wa dunia wa
ujasiliamali ulioikuza zaidi Kenya kuwa kitovu
cha teknolojia Afrika, Global Entrepreneurship
Summit (GES). Yapo mengi yalizungumziwa
kwenye mkutano huo ikiwemo kuskuma
wakinadada (wanawake) kwenye nyanja ya
ujsiliamari-teknolojia. Kufuatia hilo na hata
kabla ya ujio wa Obama, kumekuwa na
ongezeko la nguvu ya kisiasa inayokubali
kwamba teknolojia ndiyo itakayakomboa
waafrika kutokana na ujinga, umasikini,
maradhi, njaa na changamoto zingine
zinazowakabili Afrika. Zaidi ya hapo, pia ni
vizuri kutambua kwamba kuna jumuia za
wanateknolojia zinazozidi kuzuka kila kona ya
Afrika. Watu wanakuja pamoja, kushirikishana
na kukuza
Kwa nini uingie huku?
Kuna biashara nyingi unazoweza kufanya na
kujinufaisha ila biashara inayohusika na
teknolojia ni bora. Kwa upande wake, faida
kubwa ni kuwa soko hili bado ni changa na
kuna fursa pana za kuwekeza na kupata faida
kubwa. Teknolojia inavuka mipaka kirahisi na
hivyo soko ni pana sana ukiwa na mawazo ya
mbali.
Unaweza ukajiuliza sasa hivi ni jinsi gani
unaweza kuingia kwenye biashara ya
teknolojia wakati hauna ujuzi wowote kwenye
kusuka ‘code’ au kutengeneza programu wala
kuunganisha vifaa vya kielektroniki. Hapa
inafaa ujue kwamba ushirikiano upo na ujuzi ni
juu yako. Kuna njia nyingi na utitiri wa taarifa
zitakazokupa urahisi wa kufanya mambo.
Ufanye Nini ili Ufanikiwe?
Moja ya njia za kufanikiwa inayoshauriwa
ukiwa na wazo la kibunifu na kiteknolojia ni
kujiunga na “Incubator hubs.” pamoja na
jumuia za wanateknolojia. Kwenye ‘hubs’
utakuta watu wa kukuongoza, kukupa
ushirikiano kwenye kukuza biashara na hata
kukupatia mtaji.
Hapa Tanzania zipo BUNI Hub na KINU!
zilizopo jijini Dar es Salaam. Hizi ‘hus’
zinaongoza kwa sasa ila zipo nyingine kadhaa
nchi nzima zinazolenga kutoa nafasi ya kukuza
vipaji na biashara za teknolojia. Kenya ipo I-
Hub, Nailab na nyingine kadhaa. Afrika kote
zipo sehemu kama hizi zinazoshirikiana
kimataifa.
Mitaji Ipo
Kuhusu mitaji, yapo mashindano na
makampuni kadhaa hapa afrika na kutoka nje.
Pia kuna watu wapo tayari kuwekeza kwenye
teknolojia kwa sababu wanaamini kwamba
biashara inaelekea huko.
Soma zaidi hapa kuona orodha ya makampuni,
incubators na mashindano yaliofanya kazi ya
kufadhili na kukuza biashara ya teknolojia
amabayo unashauriwa kufuatilia mwaka huu.
Katika dunia ya sasa, biashara ya teknolojia
inazidi kuwa rahisi kuanzisha na kumudu.
Teknokona inakushauri ufikirie na kuthubutu
kuanzisha biashara kwenye uwanja huu. Je,
una mawazo zaidi ungependa kuwasilisha?
Ungana nasi.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post