Jinsi ya Kuangalia kama Simu ni Feki au La!

Hivi karibuni zilisambaa taarifa kwamba simu
feki zote nchini Tanzania zitazimwa ifikapo
mwezi Juni mwaka 2016, makala hii
itakuonesha jinsi ya kuangalia kama simu
yako ni feki ama la.
Hatukuweza kuthibisha moja kwa moja
kwamba kweli simu zitazimwa mwezi Juni
lakini tumejiridhisha kuwa kutakuwa na hatua
dhidi ya wanaomiliki simu feki pindi
itakapofika tarehe hiyo.
Zifuatazo ni hatua unazoweza kuzitumia
kuangalia kama simu yako ni fake, hakuna
mahitaji makubwa kufanya hili ila tu unahitaji
simu yako unayoitumia na unayotaka
kuiangalia.
Jinsi ya angalia IMEI namba
Andika *#06# kisha bonyeza kitufe cha
kupiga
Baada ya hapo simu yako itakuletea
IMEI namba ambapo kama simu yako
au kifaa chako kina laini mbili basi
kutakuwa na IMEI namba mbili
Namba hii pia unaweza kuipata katika
boksi la simu ama nyuma ya ya simu
hiyo baada ya kutoa betri, utaijua kwa
kuwa huwa ni tarakimu 15.
Nakili namba hizo pembeni.
Mfano wa IMEI namba iliyopatikana kwa
kupiga *#06#
Jinsi ya kuangalia kifaa kama ni feki ama
halali
Iandike ile namba uliyo nakili katika
hatua iliyopita katika sehemu ya
kuandikia ujumbe (SMS)
Utume ujumbe huo kwenda namba
15090
Baada ya kutuma meseji hiyo
utaangaliziwa je hiyo IMEI namba ni ya
simu ya aina gani na nani mtengenezaji
wa simu hiyo.
Subiri majibu (haitachukua muda
mrefu)
Ujumbe huo ukija unakuwa na maelezo
ya kampuni iliyotengeneza simu hiyo
pamoja na jina la simu hiyo.
Mfano wa ujumbe unarudishwa baada ya
kutuma IMEI namba
Jinsi ya kujua kama simu yako ni feki
Kama jina la mtengenezaji wa simu yako
pamoja na aina ya simu yako (Uliyo jibiwa
baada ya kutuma IMEI namba) haviendani na
majina ya simu yako (ambayo yameandikwa
katika simu yako) basi ujue simu yako
inamashaka na ni vyema kumuuliza muuzaji
wako juu ya hilo.
Kama majina yaliyorudi hayaendani na majina
yaliyoandikwa katika simu yako basi upo katika
kundi lenye uwezekano wa kuwa na matatizo,
TUNAKUSHAURI ufuate utaratibu na
kuibadilisha ama kuacha kuitumia simu hiyo
kabla ya mwezi Juni.
Kwanini TCRA wanataka tubadilishe simu
Vyombo vya usalama vinaweza kukamata
wahalifu wa kutumia mitandao ya simu kwa
msaada wa IMEI namba hivyo mtu akiwa
anatumia simu ambayo haina au ina IMEI
namba ambayo sio sahihi anazuia utendaji
kazi wa taasisi za usalama hivyo wao kama
mamlaka wanatakiwa kuhakikisha kila mtu
anatumia simu yenye IMEI namba sahihi.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post