Bodi ya mikopo ya elimu ya juu yajipanga kutatua kero za wanafunzi.

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini imesema
kwasasa imekwishaimarisha mifumo yake ya
kupokea na kushuhulikia malalamiko ya
wanafunzi haswa kwa waliokosa mikopo kwenye
bodi hiyo.
Hayo yamebainiswa na meneja wa habari, elimu
na mawasiliano wa bodi hiyo Bwana Omega
Ngole huku akisema bodi hiyo kwasasa
imejipanga vyema katika kuhakikisha wanafunzi
wanaomba mikopo wanapata mikopo kwa wakati.
Bwana Omega Ngole ametoa wito kwa mafisa
mikopo wa vyuo hapa nchini kuhakikisha
wanabainisha matatizo ya wanavyuo na
kuyashuhulikia kwa wakati ili kupunguza
migogoro ya wanavyuo hao katika upatikanaji wa
mikopo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post