Zaidi ya askari mgambo 50 waliosimamia mtihani
wa kidato cha nne Novemba 2 mwaka jana katika
shule 47 za sekondari za halmashauri ya
manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza
wamevamia ofisi ya mkurugenzi wa manispaa
hiyo wakishinikiza kulipwa madai yao zaidi ya
shilingi milioni 30, huku polisi waliokuwa na
silaha za moto pamoja na mabomu ya machozi
wakilazimika kuwatawanya ili kuimarisha ulinzi
katika ofisi hizo.
Askari mgambo hao wakiwa wamevalia kombati
zao, walianza kuwasili katika ofisi za halmashauri
ya manispaa ya Ilemela kuanzia majira ya saa
moja asubuhi, wakiwa na matumaini ya kulipwa
madai yao ambayo wamekuwa wakiahidiwa kila
mara na mkurugenzi wa manispaa hiyo John
Wanga, lakini walijikuta matumaini yao
yakiyeyuka ghafla mithili ya umande wa alfajiri
ilipofika majira ya saa kumi na moja na nusu jioni
baada ya kuitiwa askari polisi waliokuwa na
silaha za moto na mabomu ya machozi kwa
lengo la kuwatawanya.
Afisa habari wa halmashauri ya manispaa ya
Ilemela Viola Mbakile akizungumza na ITV kwa
njia ya simu kwa niaba ya mkurugenzi wa
manispaa hiyo amesema askari mgambo hao na
baadhi ya askari polisi waliosimamia mtihani huo
wa kidato cha nne kwa muda wa wiki tatu
kuanzia tarehe 2 hadi 27 Novemba mwaka jana,
watalipwa stahiki zao Jumamosi Februari 6 na
kila mmoja anatakiwa kwenda na kitambulisho
chake, huku afisa elimu sekondari Juma
Kasandiko akipata kigugumizi cha kueleza
sababu zilizomfanya kuwaita askari polisi ili
kuwatawanya baadhi ya askari mgambo hao
walioamua kupiga kambi katika ofisi za manispaa
hiyo.
› Askari mgambo Ilemela wavamia ofisi ya
mkurugenzi kudai posho zao.
2
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon