Idara ya uhamiaji mkoa wa Morogoro
imewafikisha mahakamani wahamiaji haramu 23
raia wa Ethiopia waliokamatwa na jeshi la polisi
mkoani humo kwa nyakati tofauti pamoja na
watuhumiwa wawili wa mtandao wa uingizaji na
usafirishaji wahamiaji hao ndani ya nchi.
Akisoma maelezo ya kesi hiyo mbele ya hakimu
mkazi mkoa wa Morogoro Agripina Kimanze kwa
niaba ya mwendesha mashitaka wa uhamiaji
Kajuna Rwelamila amesema kesi hiyo
haikusikilizwa kutokana na washitakiwa kuwa
raia wa kigeni na hawafahamu lugha ya
kingereza wala kiswahili na hivyo kuahirishwa
hadi februali 18 mwaka huu watakapopata
mkalimani wa lugha.
Kaimu afisa uhamiaaji mkoa wa Morogoro naibu
kamishina Josephat Malumbu amesema idara
hiyo imejipanga kuhakikisha inapambana watu
wanaosafirisha wahamiaji haramu na kwamba
katika mtandao wa uingizaji na usafirishaji
wahamiaji hao wamo viongozi wa serikali na
kuwa hatawafumbia macho walewote
watakaokamatwa wakifanya biashara hiyo.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon