Watu wawili wamefariki dunia wakati wakivua
samaki katika mto Ruvuma huko Mkenda
mpakani mwa Tanzania na Msumbiji ambapo
mwili wa mtu mmoja umepatikana huku
wananchi wakiendelea kuutafuta mwili mwingine.
Watu waliofariki katika mtu Ruvuma wametajwa
kuwa ni Said Mapanja ambaye mwili wake
umeshapatikana na Bruno Ngaponda ambaye
mwili wake bado unatafutwa na wote wana
miaka thelasini na mbili ambapo ITV
imezungumza na baba mzazi wa marehemu
Bruno Bw. Edmund Ngaponda ambaye anaeleza
jitihada zinazofanyika katika kusaka mwili wa
mwanae katika mto Ruvuma hadi mto msinji
unaokutana na mto Ruvuma.
Wananchi waishio mpakani mwa Tanzania na
Msumbiji katika maeneo ya Nakawale na Mkenda
wanasema kuna vifo vingi vinatokea katika mto
huo ambapo ndani ya miaka mitano watu zaidi ya
kumi wamekufa katika mto Ruvuma na hakuna
viongozi wa serikali wanaowatembelea kuwapa
pole hivyo wameipongeza ITV kwa
kuwatembelea.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma
kamishna msaidizi wa Polisi ACP Zuberi
Mwombeji amesema taarifa za watu kufa maji
mto Ruvuma bado hajazipata na hivyo atafuatilia
tukio hilo.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon