Moja kati ya maendeleo yaliyofanyika katika
kipindi cha miaka iliyopita ni jinsi ambavyo
teknolojia inavyo weka urahisi wa watu
kujichanganya na dunia nzima kwa ujumla.
Kwa mfano kama mtu amezaliwa kiziwi
anaweza pata vifaa maalum vya kiteknolojia
vitakavyoweza kumuwezesha kusikia bila
shida yeyote.
Kama mtu hawezi tembea pia kuna vifaa
maalumu vya kumuwezesha kutembea
(exoskeletons). Kuna mambo mengi sana
yaliyorahishishwa kwa kutumia teknolojia. Hata
kama una wakati mgumu katika kuhamisha
mouse ya komyuta yako, kuna njia ya
kukuwezesha kutumia mouse (kwa kutumia
Animouse) hiyo bila shida yoyote.
Njia hii itafanya kazi kwa wale wanaopata
wakati mgumu katika kutumia mouse za
kompyuta zao (laptop sana sana) na hii
ikijumuisha hata wale ambao mouse zao za
laptop zimekufa
Programu moja ya bure na rahisi kutumia
inayoitwa Animouse itakuwezesha kufanya
hivyo. Programu hii imeanzishwa na mvulana
mdogo tuu, kwa lengo la kuwawezesha watu
walio na ulemavu (mikono) kuweza kutumia
mouse bila kuwa na tatizo
Animouse inatumia WebCam ya Kompyuta
yako na ‘Software’ ya kubashiri sura (Facial
recognition) ili kuitafuta sura yako katika
kufanya kazi
Mara tuu Animouse inapokupata, itapeleka
msale wa mouse (cursor) sawa sawa na
sehemu ambayo utakuwa ukipeleka kichwa
chako katika kompyuta (kulia,kushoto,juu au
chini)
Muhimu: Animouse ni program ambayo ni ya
bure kabisaa! Na inapatikana katika njia ya
wazi (Open source) hii ikiwa inamaanisha
kwamba kama programa mwingine anataka
kuiboresha au kufanya baadhi ya maboresho,
anaruhusiwa. Animouse inafanya kazi kwenye
kompyuta za Windows tuu.
JINSI YA KUSHUSHA/KUPAKUA
Bofya Hapa Kuingia katika mtandao wa mouse
hiyo na kisha click file la kudownload ambalo
lina Zip yaani ‘Download Animouse Zip‘.
Ukishamaliza shusha faili hilo fungua faili lako
la zip, kisha tafuta App ya Animouse na baada
ya hapo yatoe katika mfumo ambao mafaili
hayo yapo (Extract). Na mwisho kabisa bofya
App ya Animouse ili kuanza kuitumia.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
Write commentsWapi sasa naipakua hii app
ReplyEmoticonEmoticon