Kwa wale wanaotumia zaidi simu
zilizotengenezwa na makampuni ya kutoka
Uchina hawatakuwa wageni na jina la Hot
Knot. Hii ni huduma ya kuhamisha mafaili
kutoka katika simu moja kwenda simu
nyingine inayofanana na mfumo wa Bluetooth.
Njia hii mpya inatumia screen za simu janja
yako kutuma na kupokea data kutoka
katika screen ya simu nyingine ambazo
zimewekwa umbali wa karibu usiozidi
sentimita moja.
Kuhamisha picha ama video.
kuhamisha mawasiliano kama vile
namba za simu na majina katika simu.
Kuhamisha data za application.
Inaweza kuwezesha Bluetooth pairing
ama kuwezesha kuunganishwa wi-fi
Inaweza kutumika katika matumizi ya
malipo kwa njia ya simu.
Jinsi njia hii inavyofanya kazi!
Hot knot inatumia chip za sensor za mguso
kutuma taarifa za mawasiliano kwa kifaa
kilichopo karibu wakati sensor za mvuto
( gravity) zinatumika kuhakikisha kuna mgusano
wa vifaa hivyo na kwa proximity sensor
zitakuwa zinatumika kuangalia kama kuna
kifaa eneo la jirani.
Hot Knot inaonekna kama ni suluhisho la
gharama naafuu kutokana na ukweli kwamba
teknolojia hii haitumiii kabisa transmitter na
receiver.
Kwanini teknolojia hii inapatikana katika simu
zinazotengenezwa China zaidi?
Wabunifu wa teknolojia hii ambao ni Media
Tek kutoka Taiwan wanamiliki hisa katika
makampuni yanayotengeneza screen za simu
huko China hivyo ilikuwa rahisi kuweza kupata
watengenezaji watakao ijaribu teknolojia hii
huko. Hata hivyo kampuni hiyo inategemea
kukua na kuufikia ulimwengu mzima.
Hata hivyo hii ni huduma inapatikana katika
simu ambazo zimewekewa hii huduma kutoka
katika kiwandani kwa maana ya kwamba
huduma hii haiwezi kupatikana kwa
kupakuliwa.
Nenda katika mpangilio (settings) wa
simu yako kisha chagua Hot Knot.
Simu yako itakuuliza kama unataka
kuruhusu huduma hii screen ikigusana
na kifaa kingine Allow data exchange
when the screen touches another
device? ukikubali utakuwa umeiwezesha
simu kuweza kuhamisha data pale
inapogusishwa na simu nyingine.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon