Zoezi la kutoa kivuko kilichozama lakutana na wakati mgumu

Licha ya kuwasili kwa mitambo kusaidia
zoezi la uokoaji wa kivuko kilichozama,
zoezi hilo limeshindwa kufanyika kwa ufanisi
kutokana na mvua kubwa iliyoanza
kunyesha toka saa saba usiku hadi majira
ya saa kumi jioni kukwamisha zoezi hilo
pamoja na juhudi za kuvuta kivuko hicho
kushindikana.
Hata hivyo huduma ya mawasilinao baina ya
upande wa Ulanga na Kilombero imeweza
kurejea mara baada ya Wizara ya
mawasilinao ujenzi na uchukuzi kufanikiwa
kutoa boti ambazo zimeanza kuvusha watu
ili waendelee na safari.
Zoezi la uokoaji na uvutaji wa kivuko ch MV
Kilombero limezidi kuwa gumu, kutokana na
changamoto ya vifaa vya uokozi, pamoja na
mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika
eneo hilo, hivyo kukwamisha juhudi
zinazoendelea kutolewa na mamlaka za
uokozi.
Licha ya kutumia helkopta ya jeshi la Polisi
kutafuta kama kuna watu ambao
walisombwa na maji, juhudi hizo zimegonga
mwamba baada ya kutopatikana kwa mtu
hata mmoja.
Hata hivyo juhudi zilizofanywa na wizara ya
uchukuzi kwa kushirikiana na vikosi vya
uokoaji kutoka kikosi cha wanamaji,
vimefanikiwa kurudisha mawasiliano ya
pande hizo mbili, kwa kuanza kuvusha
wananchi wa kilombero na ulanga kwa
kutumia boti za mwendo kasi. .
Wananchi wameiomba serikali kuongeza
jitihada katika zoezi la uokoaji, na
kuishukuru kwa kutoa boti ambazo
zimeanza kuvusha watu.
Zoezi la kukitoa kivuko na kukivuta nchi
kavu limeshindikana kwa siku ya jana
kutokana na kunyesha kwa mvua hiyo
pamoja na mitambo iliyopelekwa kuvuta,
kushindwa kufanikiwa.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post