Wahitimu wa vyuo vikuu nchini wametakiwa
kuondokana na dhana ya kuchagua kazi za
kufanya pindi wamalizapo masomo ya fani
wanazosomea na badala yake watumie
fursa zilizopo kujiongezea ujuzi wa kufanya
kazi.
Rai hiyo imetolewa kufuatia wasomi wengi
kudaiwa kushindwa kuajiriwa kwa kukosa
ujuzi wa fani walizosomea.
Ni katika mkutano wa wajasiriamali na
wakufunzi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe ,
ambapo Prof Ganka Nyamsoro, Mkuu wa
Chuo cha Mzumbe Tawi la Dar Es Salaam
amesema, chuo hicho kimechaguliwa
kusimamia mradi wa kuwasaidia wahitimu
kupata nafasi katika kampuni za
wajasiriamali ili waweze kujiongezea
uzoefu na kupata ajira.
Mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la SWEDENI
umelenga kutoa fursa kwa wahitimu wa
vyuo vya elimu ya juu kupata uzoefu wa
yale waliyosomea chuoni.
Kwa upande wa Wajasiriamali hao wadogo
na kati wamesema kwao ni Fursa Muhimu
Kwakuwa watafanya kazi na watu wenye
Taaluma,Huku wahitimu nao wakipata ujuzi
kutoka kwao.
Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la ajira
mbali na kuwa Serikali imejitahidi kuwekeza
katika elimu.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon