Rais amwapisha Luteni Jenerali Venance Mabeyo

Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dr John Magufuli
amemwapisha Lutenia Jenerali Venance
Mabeyo kuwa mnadhimu Mkuu wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi (JWTZ) pamoja na
kuwateua maafisa wakuu wengine wa jeshi
kushika nyadhifa mbalimbali.
Luteni Jenerali Venance Mabeyo ameshika
nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali
Ndomba ambaye alistaafu Disemba 31,
mwaka jana.
Mapema Januari 30, Ikulu Jijini Dar Es
Salaam Rais John Magufuli amemwapisha
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi Lutein Jenerali Venance Mabeyo
pamoja na viongozi wengine.
Akizungumzia uteuzi wa maafisa wakuu
walioteuliwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na
Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange
amesema maafisa hao ni pamoja na Meja
Jenerali James Mwakibolwa ambaye
amekuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la
Nchi kavu kuziba nafasi iliyoachwa wazi na
Meja Jenarali Salum Mustafa Kijuu, Meja
Jenerali Yakub Sirakwi anakuwa Mkuu wa
Chuo cha Ulinzi wa Taifa kuchukua nafasi
iliyoachwa wazi na Gaudence Milanzi
ambaye amateuliwa kuwa Katibu Mkuu
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Wengine walioteuliwa na Rais ni aliyekuwa
afisa mnadhimu katika makao makuu
kamandi ya Jeshi la Anga Brigedia Jenerali
George Ingram ambaye ameteuliwa kuwa
Mkuu wa Kamandi hiyo, Brigedia Jenerali
Jacob Kingu amekuwa Mkuu wa Shirika la
Mzinga.
Brigedia Jenerali Robinson Mwanjela
amekuwa Mkuu wa Chuo cha tiba Lugalo,
Brigedia Jenerali George Msongole
amekuwa Kamanda wa Brigedi ya Tembo
na Brigedia Jenerali Sylvester Minja ambaye
amekuwa Mkuu wa chuo cha Ukamanda na
unadhimu na wote wameshika nafasi
zilizoachwa wazi baada ya waliokuwa
wakishika nyadhifa hizo kustaafu.
Wakati huo huo Rais na Amiri jeshi mkuu Dr
Magufuli amembakisha jeshini Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange
ambaye alitakiwa kumaliza muda wake
January 30 mwaka huu.
Aidha mkuu wa majeshi Davis
Mwamunyange ametumia nafasi hiyo
kuwapongeza maafisa wakuu wote
walioteuliwa.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post