Kampuni ya huduma za meli MSC inayotoa
huduma zake katika ziwa Victoria
imewatahadhariasha wavuvi wanaofanyia
shughuli zao ndani ya ziwa hilo kuacha
kutega nyavu kwenye maeneo ya njia za
meli kwa ajili ya usalama wao na meli.
Tahadhari hiyo imetolewa kufuatia Meli ya
Mv Serengeti iliyosimama kutoa huduma
zake tangu Januari 08 mwaka huu kutokana
na kupata hitilafu katika mfumo wa shafti
na majembe upande wa kulia ikiwa safarini
kuelekea Bandari ya Bukoba Januari 06
mwaka huu ikitokea Mwanza ambapo hivi
sasa imeanza kurejesha huduma zake
Kaimu meneja masoko biashara wa
kampuni hiyo Kapteni Winton Mwassa
ametoa wito huo wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Mwanza baada ya
meli ya MV.Serengeti kufanyiwa
matengenezo na kuanza safari zake kutoka
Mwanza kuelekea Bukoba
Aidha Kapteni Mwassa amesema
anatambua kuwa wanaotumia usafiri wa
meli za kampuni hiyo wamepata usumbufu
kutokana na hitilafu ya meli hiyo na
kuwadhibitishia Watanzania kuwa hivi sasa
MV.Serengeti ni salama kwa ajili ya usafiri
wa abiria na mizigo
Hii siyo mara ya kwanza kwa meli za
kampuni hiyo kupata hitilafu katika mifumo
yake ya uendeshaji na kusababisha hasara
kwa kampuni na usumbufu kwa abiria
wanaotumia huduma hiyo.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon