Fedha za Mgodi wa Buzwagi zawaponza vigogo watano

Baraza la madiwani limeagiza
wasimamishwe kazi kupisha
uchunguzi dhidi yao Kahama. Fedha za ushuru wa
huduma zilizotolewa na Mgodi wa
Buzwagi mwaka jana, zimewaponza
vigogo watano wa Halmashauri ya
Mji wa Kahama, mkoani Shinyanga
baada ya Baraza la Madiwani
kuwasimamisha kazi kwa kudaiwa
kuzitumia vibaya kwa maslahi
binafsi.
Hatua hiyo ilikuja baada ya
kujiridhisha na taarifa ya kamati ya
uchunguzi iliyoundwa na Mkuu wa
Wilaya ya Kahama, Vita Kawawa
kuonyesha zaidi ya Sh800 milioni
kati ya Sh1.6 bilioni hazijulikani
ziliko.
Miongoni mwa watumishi hao yumo
aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo kabla ya
kuhamishiwa Halmashauri ya
Longido mkoani Manyara, Felix
Kimario na aliyekuwa Mhandisi
Mkuu wa Halmashauri ambaye
alihamishiwa Halmashauri ya
Nanyumbu mkoani Mtwara, Msumba
Msoka.
Viongozi wengine waliosimamishwa
kazi na baraza hilo ni pamoja na
Mweka Hazina wa Halmashauri,
Wilfred Kisheri na Mhasibu wake,
Alex Mroso kwa kudaiwa kushindwa
kutoa takwimu sahihi ya kampuni za
nje zinazofanya kazi ndani ya mgodi
huo na kusababisha hasara ya Sh400
milioni pamoja na Ofisa Biashara wa
Halmashauri hiyo, Elius Mollel.
Katika tuhuma hizo, yumo pia Katibu
wa Bodi ya Zabuni, Joseph Maziku
ambaye ni Ofisa Ugavi wa
Halmashauri hiyo, kwa pamoja, juzi
walisimamishwa kazi kupisha
uchunguzi ambao kwa mujibu wa
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,
Abel Shija utafanywa na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru).
Kabla ya kusimamishwa kazi vigogo
hao, Kawawa aliwataka madiwani
kuhakikisha wanachukua hatua kali
za kisheria dhidi yao kwa
kuisababishia hasara Halmashauri
hiyo.
Kawawa alitoa kauli hiyo alipokuwa
akiwasilisha taarifa ya kamati yake
ya uchunguzi aliyoiunda kuchunguza
matumizi mabaya ya fedha hizo
ambazo zingetumika kwenye miradi
iliyotekelezwa chini ya viwango.
Kawawa alisema Idara ya Fedha
chini ya Mweka Hazina wake,
Kisheri, ilitoa takwimu za kampuni
17 badala ya 168 za nje zinazofanya
kazi ndani ya mgodi huo.
Akitangaza uamuzi wa
kuwasimamisha kazi watumishi hao,
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,
Abel Shija alisema Baraza limeridhia
na watumishi wengine watano
watakuwa chini ya uangalizi.
Watumishi hao ni wajumbe wa bodi
ya zabuni wanaodaiwa kushiriki
kutoa zabuni hewa kwa kampuni
hizo.
“Tunaendelea kuangalia nyendo zao
na kama watabainika walishiriki,
watachukuliwa hatua pia,” alisema

Previous
Next Post »

Ads Inside Post