Uchakachuaji wa mafuta wapungua kutoka 78% – 7%

Mamkala ya udhibiti wa nishati na maji
nchini (EWURA) imepunguza kiwango cha
uchakachuaji wa nishati ya mafuta kutoka
kiwango cha asilimia 78 mwaka 2007 hadi
kufikia kiwango cha asilimia 7 cha hivi sasa
kwa kuweka vinasaba kwenye mafuta.
Kauli hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya
Petroli Nchini Godwin Samwel ameitoa mjini
Tabora alipokuwa akizungumza na
wafanyabiashara ya mafuta kutoa mikoa ya
Shinyanga, Kigoma na Tabora.
Kufuatia hatua hiyo Mkurugenzi wa Idara ya
Petroli Nchini–(EWURA) Godwin Samwel,
amesema Mamlaka hiyo itaendelea kuweka
vinasaba katika mafuta ili kudhibiti ubora wa
Bidhaa ya mafuta kwa manufa ya
wafanyabiashara, watumiaji na Taifa.
Katika semina hiyo ya wafanyabiashara wa
mafuta kanda ya magharibi wamemlalamikia
mdhabuni anaeweka vinasaba katika mafuta
kwa kuweka kiwango kidogo cha vinasaba
na kupelekea wafanyabiashara kutozwa faini
na Ewura.
Madereva wa magari na vyombo vingine vya
moto wameitaka serikali kuendelea kudhibiti
uchakachuaji wa mafuta kwa kuwa
umepelekea magari mengi kuharibika.
Mkurugenzi wa Idara ya Petroli Samwel
amewataka wafanyabiashara ya mafuta
kufuata sheria na kanuni za uzaji wa mafuta
kama serikali ilivyoamua kuweka vinasaba
katika mafuta ya Petroli, Dizeli na mafuta ya
taa.
Ewura imesema itaendelea kukagua
shehena za mafuta yanayoingia nchini ili
kutambua ubora wake yatakayo bainika sio
bora hayato shushwa kama zaidi ya tani
39,000 za mafuta ambazo zilibainika
zimechakachuliwa na kurudisha katika nchi
yalikotoka.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post