Watu wanaodaiwa kuwa ni Majangili wametungua helkopta na kuua rubani Serengeti.

Watu wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji
haramu wameitungua kwa risasi helkopta ya
doria ya wanyamapori katika pori la akiba la
maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu
kusini mwa hifadhi ya taifa ya Serengeti na
kumuua rubani wa helkopita na kumjeruhi askari
mmoja wa wanayamapori.
Kufuatia tukio hilo, waziri wa maliasili na utalii
Profesa Jumanne Maghembe amefika katika
eneo la tukio na kusisitiza kwamba serikali kwa
kushirikiana na vyombo vyote vya dola na
vyombo vya ulinzi na usalama inaanzisha mkakati
mpya wa kupambana na ujangili na uwindaji
haramu wa maliasili ikiwemo Tembo ambao ni
rasilimali muhimu kwa taifa na kwa uhifadhi wa
taifa la Tanzania.
Waziri Maghembe ambae amefika kwenye eneo
hilo ilipotunguliwa helkopita hiyo katika safari
iliyokuwa na msukosuko mingi ya barabara na
hasa kipindi hiki cha mvua na kuikuta helkopita
iliyokuwa inarushwa na kepten Roger Gower raia
wa Uingereza ambae alifariki baada ya
kujeruhiwa kwa risasi amesema tukio hilo
limewakera wadau wote wa uhifadhi na serikali
kwa ujumla na kamwe haliwezi kuachwa lipite
bila hatua madhubuti kuchukuliwa huku
akiwaonya baadhi ya watumishi wa serikali na
askari wa wanyamapori wanaoshirikiana na
wahalifu kuwa sasa kiama chao kimefika.
Nae kamanda wa upelelezi wa mkoa wa Simiyu
Jonathan Shana amesema tukio hilo lilitokea jana
jioni wakati helkopita hiyo ikiwa katika doria
baada ya kusikika milio ya risasi ya majangili
katika pori hilo ambapo Tembo watatu waliuwawa
na kwamba watu watatu wanashikiliwa na polisi
wakihojiwa kufuatia tukio hilo ambapo
mkurugenzi mkuu shirika la hifadhi za taifa
Tanzania Tanapa Allan Kijazi amesisistiza
umuhimu wa wadau kuongeza nguvu katika
kukabiliana na matatizo ya ujangili nchini.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post