Mtu mmoja auwawa kwa kuchinjwa na kufungiwa ndani ya mashine ya kusaga nafaka Geita.

Zoezi la usafi wa mazingira katika kijiji cha
Muungano nje kidogo ya mji wa chato mkoani
Geita limeingiwa dosali baada ya tukio la mtu
mmoja kuuwawa kwa kuchinjwa na kufungiwa
ndani ya mashine ya kusaga nafaka hali
iliyosababisha mamia ya watu kufurika
kushuhudia tukio la kusikitisha na kuacha
kufanya usafi kwenye maeneo yao.
Mwandishi ameshuhudia mamia ya watu wakiwa
wamefurika katika mashine ya kusaga nafaka
inayomilikiwa na Bi.Jamira Abdu Mkazi wa chato
ambaye amemtaja marehemu kuwa anafahamika
kwa jina la Juma Saidi alikuwa akifanya kazi ya
kusaga nafaka katika mashine hiyo zaidi ya
miaka saba na kusema kwamba hivi karibuni
marehemu alikuwa na ugomvi na mkewake
ambapo alihama nyumbani kwake na kuanza
kulala mashineni hapo.
Baadhi ya wananchi wanaomfahamu marehemu
Juma wamesikitishwa na tukio la mauaji ya
kinyama na kuiomba serikali kuimalisha ulinzi na
wengine wakuiomba kurejeshwa kwa jeshi la jadi
Sungusungu kwa lengo la kukomesha matukio ya
kihalifu.
Alipotakiwa kuthibitisha tukio hilo mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu
wa wilaya ya Chato Bw. Shabani Ntalambe
hakuwa tayali kuzungumzia suala hilo kwa madai
kuwa anasimamia usafi wa mazingira ambapo
ITV imelazimika kuzungumza na afisa mtendaji
wa kijiji cha Muungano na diwani wa kata ya
Muungano ambao wamethibitisha kutokea kwa
mauaji ya kinyama.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post