Watu kumi wamelazwa kwa kuugua ugonjwa wa kipindupindu, wilayani Itilima, Simiyu.

Watu kumi wamelazwa wilayani Itilima mkoani
Simiyu baada ya kuugua ugonjwa wa
kipindupindu wilaya ambayo haikuwa na mgonjwa
hata mmoja tangu kuripotiwa kwa ugonjwa
mkoani humo mwezi desemba mwaka jana huku
zaidi ya visima 130 vikiwekewa dawa ya kutibu
maji aina Chlorine ambapo tayari kambi tatu
zimeshaandaliwa kwaajili ya kulaza wagonjwa
hao.
Akitoa taarifa ya ugonjwa wa kipindupindu katika
kikao cha kawaida cha baraza la madiwani,
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Itilima
Bw John Lyimo amesema Jan 27 wagonjwa
wameongezeka na kufikia 7 ambapo Jan 28
asubuhi wameongezeka watatu na kufikia kumi.
Baadhi ya madiwani wamesema kuwa ni wajibu
kama wawakilishi wa wananchi kuhakikisha
wanawahamasisha wazingatie usafi katika
maeneo wanaoishi ili ugonjwa huo usisababishe
vifo.
Kambi zimetengwa katika maghala ya pamba
Nangale, Ikindilo na Madilana katika jengo la
zahanati linaloendelea kujengwa tayari wilaya ya
Bariadi na Busega zimekumbwa na ugonjwa huo
tangu desemba mwaka jana.
Wakati wilaya ya Itilima ikiwa na wagonjwa kumi
hadi jana katika wilaya ya Bariadi ilikuwa na
wagonjwa nane huku hali ya usafi ikiwa bado si
ya kuridhisha ambapo bado magenge
yanaendelea kuuza vyakula katika mazingira ya
uchafu hali inayoonyesha kuwa ugonjwa huo
utaendelea kupiga kambi katika wilaya hiyo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post