Mwili wa mtu mmoja umeopolewa mto Kilombero
mkoani Morogoro katika juhudi zinazoendelea
mpaka sasa za uokozi baada ya kivuko cha MV 2
kuzama juzi.
Kwa mujibu wa mwandishi weyu Sifuni Mshana
aliyeko eneo la tukio mwili huo umeopolewa
baada ya juhudi za wananchi wa kawaida
waliojitolea kuzamia kwa ajili ya kusaidia
shughuli hiyo ya uokozi.
Hata hivyo kikosi cha jeshi la wanamaji kimefika
eneo la tukio na halijafanikiwa kuokoa mtu yeyote
mpaka sasa japo wanaendelea na harakati hizo.
Idadi ya watu isiyo fahamika mara moja
wanahofiwa kufa maji yakiwemo magari matatu
kudumbukia baada ya kivuko cha MV 2 Kilombero
kuzama katikati ya mto Kilombero kufuatia upepo
mkali.
Ulioambatana na mvua kubwa kunyesha juzi
majira ya saa moja na nusu.
Uncategories
Mwili wa mtu 1 umeopolewa mto Kilombero
katika juhudi za uokozi baada ya kivuko cha
MV 2 kuzama.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon