Mkuu wa Shule ya Sekondari Komakya avuliwa madaraka

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Novatus
Makunga amelazimika kumvua madaraka
mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari
Komakya iliyoko Mkoani Kilimanjaro kufuatia
kukiuka maagizo ya Mkuu wa Mkoa ya
kuwa vikao vyote vinavyohusiana na
michango ya wanafunzi kati ya wazazi na
uongozi wa shule kutolewa ufafanuzi kabla
michango hiyo haijaanza kukusanywa
Hatua hiyo imekuja kufuatia simtofahamu
iliyojitokeza kati ya wazazi wa wanafunzi
na uongozi wa shule uliotolewa ya kwamba
kabla ya michango kukusanywa ni lazima
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupewa Taarifa.
Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya
Sekondari Komakya iko umbali wa km 18
kutoka moshi mjini amelalama kuhusu
kupoteza muda mwingi akifuatilia ada.
Sintofahamu ilijitokeza kwa wazazi wa
wanafunzi wa shule hiyo mara baada tu
walimu wa shule iyo kuwarudisha ada
wanafunzi huku wakitaka kupewa ufafanuzi
kuhusiana tamko la mh. Rais kuhusu elimu
bure
Kufuatia suala hilo Mkuu wa wilaya ya
Moshi mjini Novatus Makunga akalazimika
kufika shuleni hapo na baada ya kusikiliza
pande zote kumvua madaraka Mkuu wa
Shule hiyo Bi.Rose Ngoti kufuatia kufanya
maamuzi na wazazi wa shule kwa
kuchangisha michango pasipo kuishirikisha
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kama waraka wa
seriklai unavyozitaka shule hizo
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mjini ina
jumla ya shule za Kata 57 wanafunzi 25,402
walimu 1300 huku changamoto kubwa ikiwa
ni upungufu wa walimu wa sayansi katika
shule hizo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post