Wafanyabiashara nchini wajipanga kujitangaza zaidi

Wakati Tanzania ikikadiriwa kuwa na
takribani futi za ujazo Trilioni 55 za gesi
asilia, na kuanza kuonekana kwenye jicho la
biashara hiyo kimataifa kama mdau muhimu
anayechipukia, wafanyabiashara kwenye
eneo hilo nao wameanza mikakati mipya
itakayowapatia fursa muhimu ya kujitangaza
kwenye soko hilo kimataifa.
Pamoja na kuwepo kwa fursa hiyo adimu,
bado kampuni nyingi za kizalendo
zinashindwa kujitangaza kwenye hatua ya
kimataifa, na chini ya mpango huo kampuni
zake zitaweza kufanyiwa tathmin na
kutambuliwa kwenye soko hilo.
Hata hivyo kuwapo kwa mtandao kama
huo, hakumaanishi kuwa awali kampuni
zilizojihusisha na uchimbaji wa mafuta,
hazikuweza kutumia fursa zilizopo kwenye
sekta hiyo.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post