Serikali yaondoa hoja ya mpango wa pili wa maendeleo Bungeni

Serikali imelazimika kuiondoa bungeni hoja
ya kujadili mpango wa pili wa maendeleo ya
taifa kwa kipindi cha miaka 5 kwa kukiuka
kanuni za bunge.
Hii ni baada ya baadhi ya wabunge kukuhoji
uhalali wa kuwasilishwa kwa hoja hiyo na
kutaka ushauri wa bunge kuhusiana na
swala hilo.
Ufafanuzi unasema Kwa kuzingatia kanuni
za bunge katika kuwasilisha hoja ili
kujadiliwa kabla ya kupitishwa na kuwa
sheria, maoni kutoka pande zote husika
yanapaswa kuzingatia, lakini iwapo hayo
hayatatekelezwa basi bunge lina uhuru wa
kuhoji uhalali wa kuwasilishwa kwa hoja
hiyo kupitia ibara ya 63, ibara ndogo ya 3
(c) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa
Tanzania.
sheria hii ikionekana kutekelezwa katika
kikao cha bunge siku ya ijumaa pale waziri
wa fedha na mipango akitakiwa kuiondoa
hoja ya kujadili mpango wa pili wa
maendeleo ya taifa kwa kipindi cha miaka
mitano.
Waziri wa fedha na mipango alilazimika
kufuata utaratibu kwa kuzingatia kanuni za
bunge kwakuondoa hoja hiyo kwakufikiwa
na idadi kubwa ya wabunge walioafikiana
kuondolewa kwa hoja hiyo
Hoja hiyo ilionekana kuzua utata katika
kikao cha asubuhi pale baadhi ya wabunge
walipojitokeza kuhoji uhalali wa
kuwasilishwa kwa hoja hiyo huku wakidai
kutohusishwa kwa pande zote husika katika
kukusanya maoni.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post