Ukosefu wa maji ya uhakika katika wilaya
ya Kishapu mkoani Shinyanga unadaiwa
kuzorotesha huduma za tiba kwenye
Hospitali ya wilaya hiyo iliyoanza kutoa
huduma novemba mwaka jana na kupewa
jina la dokta Jakaya Kikwete
Hali hiyo imebainika wakati wa shirika la
Good Neighbos lilipokuwa linakabidhi
msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya
zaidi ya milioni 220 kwa ajili ya Hospitali ya
wilaya ya Kishapu
Ni wakazi takribani laki tatu wakitegemea
matibabu kutoka katika Hospitali ya wilaya
ya Jakaya Kikwete Kishapu lakini
changamoto iliyopo kwenye hospitali hiyo ni
uhaba wa maji na kusababisha huduma
kuzolota
Mkuu wa wilaya Bi Hawa Nghumbi na
mganga mfawidhi wa Hospitali Gong Homa
Henry wamesema maji katika wilaya hiyo
pamoja na Hospitali imekuwa ni
changamoto kubwa kwa wakazi wake.
Hata hivyo pamoja na changamoto hiyo
shirika lisilokuwa la kiselikali la Good
Neighbor kupitia kwa mkurugenzi wake
Inseok Lee wametoa msaada wa vifaa tiba
vyenye thamani ya zaidi ya milioni 220
Hospitali ya Dk Kikwete ina watumishi 37
wa kada mbalimbali wakati upungufu
watumishi 163.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon