Uhamiaji Geita yaombwa kuelekeza nguvu vijijini

Idara ya Uhamiaji Wilayani Geita imeombwa
kuelekeza nguvu zake katika vijiji
mbalimbali ambako kunadaiwa kuwa na
wahamiaji haramu wanaodaiwa kufanya
shughuli mbalimbali kinyume na taratibu za
nchi hali inayotia wasiwasi kutokana na
mkoa wa Geita kuwa na matukio ya uhalifu.
Kutokana na hali hiyo Idara ya uhamiaji
Wilayani Geita imetakiwa kulifuatilia kwa
kina suala hilo na kuwaondoa wahamiaji
katika maeneo hayo.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la
Madiwa ni Wilaya ya Geita Angelo Komanya
amesema wahamiaji hao wamevamia msitu
wa Rwande na kuharibu mazingira kwa
shughuli mbali mbali wanazozifanya.
Afisa uhamiaji Wilaya ya Geita Vitalis
Komanya amesema ni kweli wahamiaji wapo
wengi katika wilaya wanatoka Ruanda na
Burundi.
Aidha wananchi wametakiwa kuacha
kuharibu mazingira kwani imeathiri
mabadiliko ya hali ya hewa

Previous
Next Post »

Ads Inside Post