Watu wawili mekamatwa katika wilaya ya
Monduli Mkoani Arusha kwa kosa la
kukutwa na meno matano ya Tembo yenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni sitini na
tano.
Shirika la hifadhi za wanyama nchini
TANAPA limesema kukamatwa kwa watu
hao kumetokana na taarifa za raia wema
zilizosaidia askari wa wanyama pori kuweka
mtego uliofanikisha zoezi hilo.
Mkurugenzi wa TANAPA Allan Kijazi
amesema mara baada ya kupata taarifa
kutoka kwa wasamaria wema kikosi cha
kiintelijesia kwa kushirikiana na wananchi
waliweka mtego wa kuwanasa watuhumiwa
hao wa ujangili ambapo wawili kati yao
walifanikiwa kutoroka.
Kufuatia tukio hilo mhifadhi mkuu wa ziwa
Manyara Domiciani Njau ametoa wito kwa
wananchi katika maeneo mbalimbali ya
hifadhi watoe taarifa kwa mamlaka husika
wanapogundua mitandao ya kiuhalifu wa
nyara za serikali
Kwa mujibu wa TANAPA pembe hizo
zilikamatwa katika eneo la Selela wilayani
Monduli majira ya saa saba kasoro usiku wa
kuamkia ijumaa iliyopita
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon