Unaitumia vipi simu-janja yako, kupiga na
kupokea simu tuu?. Inasemekana asilimia 80
ya watumiaji wa simu-janja hawatumii simu
zao katika asilimia 100 kama inavyotakiwa.
wengi huwa wanadownload vitu mbali mbali
kama magemu na mitandao ya kijamii na
kuingia katika intaneti tuu na wanakua
wameridhika. vipi kama kuna vitu vingi
unavyoweza tumia ukiwa na simu yako? Basi
unakosa vitu vingi sana unavyoweza tumia
ukiwa na simu-janja yako.
Sasa fahamu ya kwamba unaweza tumia simu
yako kama vifaa vifuatavyo,
1. Tumia Simu-janja Yako Kama Redio Za
Mawasiliano (Redio Kolu)
Aplikesheni kama zello ( Android , iPhone/
iPad,Windows) na HeyTell ( iPhone , Android ,
Windows) zinasaidi kukuwezesha kutumia
simu-janja yako kama redio kolu.
zinakuwezesha kutuma meseji za sauti za
kugusa na kuongea (push-to-talk) kama redio
kolu za ukweli
2. Tumia Simu-Janja Yako Kama Kama
Remoti Ya Kimataifa
Uamini au usiamini aplikesheni kama IR
Remote ( Android ) na Dijit ( iPhone ) zinaweza
kukuwezesha kutumia simu-janja yako kama
remoti katika vifaa mbalimbali vya ki
elektroniki. Kujua zaidi kuhusu kutumia simu
yako kama remoti soma hapa
3. Tumia Simu-Janja Yako Kama Wireless
Mouse/Keyboard/Touchpad
Je ushawahi kuwaza kununua ‘wireless
keyboard’ au ‘mouse’ lakini ukawa huna hela
ya kutosha?. sasa mtandao
kama Remotemouse.net unaweza ukakusaidia
na ukashusha aplikesheni hiyo kwenye simu
yako ya Android au iPhone na pia udownload
Aplikesheni nyingine kwa kompyuta yako ili
kutumia.
4. Tumia Simu-janja Yako Kama WebCam
Ushawahi kukaa na kufikiria kitu kama hiki
(ha!). Unaweza usijue lakini ndio hivyo
unaweza fanya simu yako ikawa WebCam ya
kompyuta yako. Kuna Aplikesheni nyingi za
bure kama WO webcam Lite ( Android )
na EpocCam ( iphone ) zinaweza kukusaidia
kutumia simu kama webcam.
5. Tumia Simu-Janja Yako Kama Wi-Fi Router
Hili linaweza lisikushangaze, simu nyingi za
Android na iphone sasa zinakuja na Wi-Fi
router ambazo zinaweza msaidia mtumiaji wa
simu hiyo kurusha mtandao wa intaneti
kwenye simu au kompyuta nyingine. ili
kuwasha na kutumia mbinu hii nenda kwenye
Wi-Fi Hotspot settings katika simu yako ya
Android au iPhone
6. Tumia Simu-janja Yako Kama GPS
Simu nyingi siku hizi zinakuja na GPS kabisa,
lakini aplikesheni kama GPS Status & Toolbox
( Android ) and Waze ( iphone ) zinaweza
kukusaidia kutumia simu yako kama GPS
kabisa.Aplikesheni hizo ni za bure katika
Appstore na Google Playstore
7. Tumia Simu-janja Yako Kama Scanner
Mara ngapi umetaka ku scan nyaraka zako na
ikakulazimu uende kwenye steshenali kwa
sababu huna scanner? Kwa kutumia Aplikeshi
ya simu yako kama CamScanner ( Android,
iPhone/iPad, Windows 8) huhitaji kuwa na
mawazo kwamba utascan wap nyaraka zako.
kitu kingine kuhusu aplikesheni hii ni kwamba
ni ya bure na unaweza kuscan na nyaraka
zako zikawa katika ubora wa hali ya juu
8. Tumia Simu-janja Yako Kama TV
KWa kutumia Aplikesheni kama LiveNow! TV
( Android ) and PBS ( iPhone) unaweza kutumia
simu yako kuangalia TV. Aplikesheni zote hizi
ni bure katika masoko ya Android na Apple
lakini unatumia Internet Kuangalia TV hiyo
katika simu.
9. Tumia Simu-Janja Yako Kama Wireless PC
Speaker
Shusha Aplikesheni kama SoundWire ( Android )
or Airfoil Speakers Touch ( iPhone, iPod, iPad)
katika simu yako na kisha shusha software ya
aplikeshi hizo katika komyuta yako. KWa
kufanya hivyo hapo utaweza kucheza miziki
katika simu yako kwa kutumia kompyuta
10. Tumia Simu-Janja Yako Kama Motion
detector
Kama simu yako ina sensa, basi unaweza
ukafanya mambo mengi ya kuvutia kama
kubadili wombo katika simu yako kwa
kupitisha mkono juu ya skrini bila kugusa simu.
kama una uhakika simu yako ina sensa basi
shusha Proximity Actions ( Android ) au Smart
Player Free ( iPhone ) kutumia simu yako bili
kugusa skrini.
Sasa nina imani unaweza kutumia Simu-janja
zako kiujanja zaidi. Kama una wazo lolote
ningependa kulisikia kuhusiana na hii makala,
tuwasiliano kupitia akaunti zetu za Twitter au
Facebook. Na No 0766598830
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
6 comments
Write commentsApplication ya kuchaji
ReplyVery nice & helpful..
ReplyAsante pia kwa saport yako
ReplyAsante pia kwa saport yako
ReplyUmeipenda eeeh
ReplyUmeipenda eeeh
ReplyEmoticonEmoticon