Njia ya Pili ya Kusoma Sms za Whatsapp bila kuonekana Tiki Za Bluu

unachukizwa na risiti za ujumbe kusomwa!?
hupendi wanao kutumia ujumbe wataarifiwe
pindi unapoufungua ujumbe huo!? Kama jibu ni
ndiyo basi upo mahali sahihi, makala hii
itakusaidia ili uweze kuondoa risiti hizi za
ujumbe kusomwa hivyo kuwaondolea uwezo
wanaokutumia ujumbe kujulishwa pindi
unapozisoma jumbe zao.
Kama ungependa unapofungua ujumbe
uliotumiwa basi yule aliyetuma ujumbe asijue
kama umeufungua basi fuata hatua
zifuatazo>>> Menu —-> Account —->Privacy
1. Nenda katika menyu kuu ya simu yako na
kisha bonyeza kwenda katika sehemu ya
mipangilio(settings)
2.Chagua Account
3.Chagua privacy
Pamoja na mambo yote ukiwa katika kurasa
hii utona sehemu iliyo andikwa read receipts
ondoa alama ya pata katika kiboksi kilichopo
mbele (kwa wanaotumia mfumo wa android)
na kama unatumia mfumo wa iOS basi
kiwashe hicho kitufe.
Angalizo hii njia haitaondoa risiti za ujumbe
unaopokelewa katika makundi ya Whatsapp hii
inamaana kwamba kama utafungua na kusoma
ujumbe unaotumwa katika makundi basi wote
walio ndani ya kundi hilo watajua muda
ulioupokea ujumbe huo.
Je wewe unaona jambo hili la mtu mwingine
kujua pale unaposoma ujumbe wake ni jambo
zuri au linaingilia faragha?

Previous
Next Post »

Ads Inside Post