MEYA WA KINONDONI

Meya mpya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar
es Salaam, Boniface Jacob, ameanza majukumu
yake mapema jana 18 Januari ya Umeya huku
akikumbana na umati wa wananchi waliofika
kumuona kwa malalamiko ya migogoro ya ardhi
ambayo ni changamoto katika Manispaa hiyo.
Hata hivyo Meya huyo baada ya kuwasili ofisini
kwake na kupokelewa na baadhi ya maafisa
kadhaa wa Manispaa hiyo na kutinga kwa mara
ya kwanza ndani ya ofisi ya Meya ambayo
atakuwa akiitumia kwa kipindi chote, baada ya
saa chache kundi la wananchi kutoka Wazo Block
B, walifika katika ofisi hiyo kwa lengo la
kumuona ilikumweleza kero zao ambazo
wamedai kuwa wafanyakazi na watendaji wa
Manispaa hiyo wamepora maeneo yao na
kuwauzia wafanyabiashara wengine.
Kwa busara ya Meya Boniface Jacob, ameweza
kusikilza kero za wananchi hao huku akiahidi
kulifuatilia suala hilo kwa ukaribu hadi hapo haki
itakapopatikana. Ambapo amewaomba
wananachi hao wasubirie kuona kama Manispaa
ilifanya tathimini na nani aliuza viwanja hivyo na
fedha ziliingia wapi ambapo ametoa agizo kwa
Mtathimini na afisa ardhi wa Manispaa kuanza
mara moja kukagua kujua nani ameusika kwenye
mgogoro.
Wakazi hao zaidi ya 50, wanaeleza kuwa,
mgogoro huo umeendelea kudumu zaidi ya miaka
15 sasa huku mara zote wamekuwa
wakizungushwa pasipo kupata haki zao. Pia
wameeleza kuwa, miongoni mwa wananchi
wanaokaa kwenye maeneo hayo wamekuwa
wakiishi kwa hofu ya kuvunjiwa nyumba zao
kwani baadhi ya watu wamekuwa wakifika na
kuwapa taarifa kuwa maeneo hayo ni ya
mwekezaji huku wengine wakitumia ubavu
kuvunja nyumba za wananchi pasipokuonyesha
hati halisi kitendo ambacho wamekiona kuwa
Watendaji wa Manispaa hiyo kuuza kinyemela
viwanja vyao.
Pia wananchi hao wamewataia baadhi ya vigogo
wa Serikali wakiwemo watendaji wa Manispaa
hiyo ya Kinondoni kwa kujimilikisha maeneo
ikiwemo kujenga nyumba katika ardhi ya
wananchi hao.

Previous
Next Post »

Ads Inside Post