Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa
wa kidato cha pili 2015 ambapo wanafunzi
324,068 sawa na asilimia 89.12 ya
watahiniwa 363,666 wamefaulu huku somo
la Kiswahili likiongoza kwa ufaulu wa
asilimia 86.34 na somo la hesabu ukiwa
chini zaidi kwa asilimia 15.21.
Miongoni mwa waliofaulu wasichana ni
164,547 sawa na asilimia 89.00 na
wavulana 159,521 sawa na asilimia 89.24
na wengine 39,567 sawa na asilimia 10.88
wameshindwa kupata alama za
kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.
Katika matokeo hayo idadi ya watahiniwa
waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya
Distinction, Merit na Credit ni 155,667 sawa
na asilimia 42.80 ambapo wasichana
wakiwa 68,780 sawa na asilimia 37.20 na
wavulana 86,887 sawa na asilimia 48.60.
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Charles
Msonde anasema tathmini ya jumla
inaonyesha ufaulu wa wastani wa juu
kwenye masomo ya msingi ya somo la
Uraia, Historia, Geografia, Kiswahili,
Kiingereza na Sayansi huku ufaulu wa chini
ya wastani ukijitokeza kwenye masomo ya
Hisabati, fizikia, Chemia na masomo ya
biashara ikilinganishwa na mwaka 2014.
Kufuatia hali hiyo Dk. Msonde anasema
jitihada zaidi zinahitajika kwa walimu ili
kuboresha ufundishaji zaidi kwa kidato cha
tatu.
Shule 10 za Sekondari zinazotajwa kuwa za
mwisho katika matokeo hayo ni Michenjele,
Makong’onda, Mkoreha za mkoani Mtwara,
Mdando, Mlongwema, Kwai, Kwalunguru na
Mlungui zote za mkoani Tanga, Furaha ya
Dar Es Salaam na Lionja ya Lindi.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon