Bandari ya Dar yadaiwa
kupisha silaha
Jan 16th, 2016 ·
Mjadala wa wazi wa kujadili mgogoro wa
Burundi unaoendelea makao makuu ya
jumuiya ya Afrika mashariki umezidi
kurindima jijini Arusha ambapo wajumbe
kutoka asasi za kiraia wameeleza kuwepo
kwa taarifa kuwa bandari za hapa nchini
zinahusika kupitisha silaha zinazokwenda
nchini Burundi hivyo wameitaka jumiya ya
Afrika mashariki kuchunguza jambo hilo ili
kubaini ukweli wake.
Madai hayo yamekuja ikiwa ni siku ya tatu
ya mijadala inayohusisha wadau
wanaohusika na mgogoro wa Burundi kwa
lengo la kutafuta suluhu nchini humo.
Katika mjadala wa leo uliohusisha makundi
ya asasi za kiraia kutoka nchi za jumuiya ya
Afrika mashariki ,wajumbe wameonesha
kutoridhishwa na kuendelea kuwepo kwa
mijadala ya muda mrefu katika kutafuta
amani ya nchi ya Burundi ili hali serikali ya
nchi hiyo bado haijaonesha nia ya dhati
katika kutafuta suluhu.
Vital Nshimirimana ni mmoja wa wajumbe
kutoka asasi za kiraia , wakati akitoa
mapendekezo katika mjadala amesema
kumekuwepo na taarifa kuwa bandari ya Dar
es salaam ya nchini hapa imekuwa
ikihusika kupitisha silaha zinazokwenda
katika baadhi ya nchi za jumuiya ikiwemo
nchi ya Burundi hivyo wameitaka kamati ya
utatuzi wa migogoro kuchunguza ili kubaini
ukweli wa mambo.
Akielezea tuhuma hiyo mwenyekiti wa
kamati ya masuala ya ndani ya utatuzi wa
migogoro katika nchi wanachama wa
jumuiya ya Afrika mashariki Abdulah Mwinyi
amesema jambo hilo ni lazima litafutiwe
ushahidi wa kutosha kwa kuwa si jambo
jepesi.
Maria Baricako kutoka taasisi ya utetezi ya
wasichana na wanawake, kuhakikisha
wanapata ulinzi na usalama katika nchi ya
Burundi amesema wamejitokeza kuhakikisha
wanapaza sauti kwa ajili watu wa Burundi
wanaohitaji kupata haki ya kuishi katika
nchi yao.
Kumekuwepo na mijadala kwa siku tatu
mfululizo ambapo baadae mapendekezo
yanayotolewa yanategemewa kupelekwa
katika bunge la Afrika mashariki kwa ajili ya
kutafutiwa ufumbuzi.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon