Mchekeshaji wa Orijino Komedi na
mjasiriamali, Masanja Mkandamizaji
amesema kila anachomiliki amekinunua kwa
pesa yake halali huku akishangaa kwanini
watu wameshtuka baada ya kuona anamiliki
BMW yenye plate namba ya jina lake.
Akizungumza katika kipindi cha 360 cha
Clouds TV Ijumaa hii, Masanja alisema
anamiliki magari mengi huku akidai BMW X6
ameinunua kama mtu mwingine anavyonunua
baiskeli. "Mimi nina magari mengi sana na
yote nayachukulia kama chombo cha usafiri
cha kunitoa point moja kwenda nyingine,”
alisema. “Sasa nashangaa watu wanaongea
sana kuhusu mimi kwani gari kitu gani! Hiyo
BMW X6 nimenunua kama watu wengine
wanavyonunua baiskeli," alijinadi.
Aliongeza, "Na hata hao TRA kama
wananisikia waje hapa Clouds nimekuja nayo
ipo hapo chini ili waangalie kama sijailipia."
Masanja alisema anafanya biashara za aina
mbalimbali hivyo kununua gari la thamani
siku kitu cha ajabu kwakuwa anaweza
kununua kupitia biashara yake moja tu.
Uncategories
MASANJA AWAAMBIA TRA WAJE WAKAGUE
GARI LAKE WAONE KAMA HAJALIPIA
USHURU...GARI YENYEWE HII
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon