IKIWA tayari Ubalozi wa Ubelgiji nchini
Tanzania umekwishatoa viza kwa
mshambuliaji Mbwana Samatta kwenda
kusaini klabu ya KRC Genk, lakini taarifa
zinasemekana kuwa huenda anaweza
akabaki TP Mazembe ya DRC kumalizia
Mkataba wake hadi Aprili.
Hiyo inatokana na Rais wa Mazembe, Moise
Katumbi kugoma kumuuza Mwanasoka huyo
Bora wa Afrika kwa wachezaji wa
ndani katika klabu hiyo Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Rais wa Klabu ya TP Mazembe, Katumbi
Moise.
Inasemekana pia kuwa, Katumbi anataka
Samatta anende kucheza Nantes FC ya Ligi
Kuu ya Ufaransa, ambayo amekwishafikia
makubaliano nayo, na kwamba wiki iliyopita
Nantes FC ilituma mwakilishi wake jijini Dar
es Salaam, ambaye alifanya mazungumzo na
Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo mbele
ya Ofisa mmoja wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF).
Katika mazungumzo, Kisongo alifikia
makubaliano ya maslahi binafsi na Samatta
ikiwemo dau la kusaini, mshahara, masharti
na marupurupu mengine. Kisongo alitaka
kiwepo kipengele cha mchezaji kutorejeshwa
Afrika iwapo hatapata nafasi ya kucheza
Nantes, bali auzwe klabu nyingine ya Ulaya
na ikakubaliwa.
Samatta hivi karibuni akikabidhi jezi yake
kwa rais Mstaafu, Dk Jakaya Kikwete wakati
Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni
na Michezo, Mh. Nape Nnauye akishuhudia
tukio hilo.
Nantes ilionesha nia ya dhati kabisa ya
kumchukua Samatta na Kisongo aliinuka
kwenye meza ya mazungumzo akiwa
amekubali na kusema anakwenda
kuzungumza na mchezaji. Hata hivyo,
inaonekana Samatta mwenyewe ndiye
anayetaka kwenda Ubelgiji na si Ufaransa,
kwani kitendo cha Kisongo kutorejesha
majibu kwa Nantes kinaashiria ameshindwa
kumshawishi mchezaji wake akubali ofa
hiyo.
Wakati huo huo, Rais wa Mazembe hayuko
tayari kumuuza Samatta Ubelgiji na yuko
tayari kuona Samatta anabaki Mazembe
kumalizia Mkataba wake ili aondoke kama
mchezaji huru Aprili, hali ambayo itamlazimu
kusubiri hadi Agosti kusaini Genk.
Kwa sasa, kambi ya Samatta inajaribu
kuomba msaada kwa viongozi wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wakazungumze na Katumbi ili akubali
kumuacha mchezaji aende klabu
aliyochagua.
Rais Mstaafu, Dk Jakaya Mrisho Kikwete
ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa chama
tawala, CCM, Waziri wa Michezo, Nape
Nnauye kwa pamoja wameahidi kumsaidia
Samatta katika suala la kumlainisha Katumbi
akubali kupokea ofa ya Genk.
Wakati huo huo, Nantes wamekuwa
wakimpigia simu Kisongo wakisema
wanamsubiri mchezaji aende kusaini, lakini
Meneja huyo anakosa majibu ya uhakika.
Inaonekana tayari Katumbi anaujua mchezo
wote unaoendelea naye ameamua kukaa
kimya akiamini Samatta hawezi kufanya
chochote kwa sasa bila baraka zake. Wazo
la kusema Samatta asubiri hadi mwezi Aprili
atakapomaliza Mkataba wake ili kusaini
kama mchezaji huru mwezi Agosti,
halifurahiwi hata na Kisongo mwenyewe.
Samatta aliyejiunga na TPM mwaka 2011
akitokea Simba SC aliyoichezea kwa nusu
msimu, akitokea African Lyon, hadi sasa
ameichezea klabu hiyo mechi 103 na
kuifungia mabao 60. Ndani ya mechi hizo,
kijana huyo wa umri wa miaka 24,
ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na
Mazembe, huku naye akiibuka mfungaji bora
wa michuano hiyo na kutwaa tuzo ya
Mchezaji Bora Anayecheza Afrika.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon