Kwa ufupi
Asilimia 90 ya vyote vinavyotokea
katika maisha yetu vinategemea
jinsi tunavyoonyesha hisia zetu.
Habari
Kanuni ya 90 kwa 10 ni muhimu na
itakusaidia katika huyabadili maisha
yako na namna unavyoyapokea au
kuyaangalia mambo na kuonyesha
hisia zako.
Kanuni hiyo ina msingi ufuatao;
asilimia 10 ya maisha yetu
inafanywa na vile vitu vinavyotokea
kwetu na tusivyoweza kabisa
kuvibadili kwa uwezo wetu.
Asilimia 90 ya vyote vinavyotokea
katika maisha yetu vinategemea jinsi
tunavyoonyesha hisia zetu.
Kamwe hatuwezi kubadili chochote
wala kugeuza chochote katika yale
yanayotokea kwetu katika ile asilimia
10% mfano, hatuwezi kubadili wala
kuzuia pale gari linapoharibika
barabarani, hatuwezi kuzuia wala
kubadili chochote pale ndege
inapochelewa kuondoka uwanjani,
hatuwezi kufanya chochote pale kitu
kinapoingilia safari yako barabarani
na kukuchelewesha, kwa mfano
foleni isiyotarajiwa.
Asilimia 90 ni tofauti. Sisi tuna
uwezo mkubwa katika kuiamua na
kubadili hali kutegemea na vile
tunavyozionyesha hisia zetu. Huwezi
kuzuia taa nyekundu inapowaka
barabarani kukuashiria usipite,
lakini waweza kuzitawala hisia zako
zinazoweza kusababishwa na taa ile.
Kamwe usimruhusu mtu au watu
wakupumbaze au kukufanya mjinga
kwa kuzichochea hisia zako. Jaribu
kujitawala na kujiweza.
Labda tutumie mfano huu;
Unapokunywa chai asubuhi na
familia yako mara binti yako
anagonga kikombe kwa bahati
mbaya na chai inamwagika na
kuchafua shati lako la jeupe la
kazini.
Hapa kwa kweli huna lolote la
kufanya kuhusu kilichotokea, (maji
yamekwisha mwagika), kinachofuata
sasa kitategemea na
utakavyozionyesha hisia zako. Je,
utalaani, utatukana, utabwata,
utampiga makofi binti yako? Kama
utamchapa, baada ya hapo labda pia
utamgeukia mke wako na
kumgombeza kwa kuweka kikombe
vibaya mezani na hapo mtaanza
kuzozana na mkeo.
Mara utaenda chumbani kubadili
shati na kwa hasira utatoka na
kumkuta binti yako akiendelea kulia
na kwa kulia na kutokunywa chai
anaachwa na gari la shule. Labda
mke wako hawezi kumpeleka binti
yako shuleni, kwa hiyo unalazimika
kumchukuwa kwa hasira
kumuwahisha shuleni, kwa sababu
umechelewa unaendesha kwa kasi
kiasi cha kusimamishwa na askari
wa barabarani na kutozwa faini.
Baada ya kucheleweshwa zaidi na
askari mnafika shuleni na mwanao
mmenuniana na kwa hasira anaruka
kutoka kwenye gari bila hata
kukuaga na kukimbilia dasani.
Unatoka na kukimbia ofisini, mara
unapoingia ofisini unakumbuka
umesahau begi lako la ofisini, kwa
sababu ulitoka chumbani kwa hasira.
Siku yako imeanza vibaya,
itaendelea vibaya na kuwa mbaya
zaidi hata mwisho wake.
Unaporudi numbani unakuta mama
na binti wote hawana amani na
wewe, kwa kile ulichokianzisha
asubuhi.
Yote haya kwa nini? Ni kwa vile
ulivyozionyesha hisia zako asubuhi.
Kwa nini siku yako imekuwa mbaya?
Je, ni chai imesababisha?
Je, ni binti yako amesababisha?
Je, ni askari wa barabarani?
Au ni wewe uliyesababisha?
Ukweli ni kwamba hukuwa na lolote
la kufanya kwa kumwagika kwa chai,
lakini jinsi ulivyoonyesha hisia
katika zile sekunde tano, ndipo
ulipoharibu siku yako. Yamkini
ingekuwa bora ungefanya tofauti
kama ifuatavyo.
Chai imemwagika katika shati lako la
kazini,
Binti yako anataka kulia kwa hofu
Taratibu mguse begani na
kumwambia asihofu kwa sababu hali
kama hizo hutokea, ila awe makini
wakati mwingine awapo mezani.
Chukua taulo haraka jifute na
kubadili shati na utoke na begi lako
la kazini na kuagana na binti yako
akienda kupanda gari la shule.
Ondoka, wahi kazini na upate dakika
chache za kusalimiana na
wafanyakazi wachache kabla ya
kuanza kazi.
Angalia tofauti hapa!
Imekuwa michakato miwili tofauti,
yote ilianza kwa tukiko moja, na yote
imeishia katika hali za tofauti.
Kwa nini? Kwa sababu ya jinsi
ulivyoonyesha hisia zako.
Hapa utaona ukweli kwamba, una
nafasi kubwa ya kuzitawala asilimia
90 za yale yanayoendelea maishani
mwako, hususan kwa jinsi
uzitawalavyo hisia zako.
Jinsi ya kuitendea kazi kanuni hii
Iwapo mtu au watu wanakusema au
kukufanyia mambo mabaya,
usiyameze na kuyaruhusu
yakuumize.
Yaruhusu yakutoke haraka kama vile
maji yanavyoachana na glasi.
Usiziruhusu semi mbovu ziumize
moyo wako. Onyesha hisia zako
kiusahihi na kwa kufanya hivyo
hautaiharibu siku yako.
Kwa kuonyesha hisia zetu vibaya
twaweza kupoteza marafiki, twaweza
kufukuzwa kazi, twaweza kuharibu
jina na sifa yetu au kujiongezea
msongo wa mawazo.
Unafanyaje pale mtu
anapokuendeshea gari vibaya au
kukuchomekea ukiwa barabarani
unaendesha, unatukana? unalaani?
Unagonga usukani au kupiga honi
kwa hasira? Je, unapofanya hivyo
kuna anayekujali? Kwa nini uruhusu
magari yaharibu raha ya uendeshaji
wako. (usisahau kanuni ya 90-10).
Umeambiwa unafukuzwa au
unapunguzwa kazi, kwanini upoteze
usingizi na kukaa ukihofu?
Inawezekana kubadili hiyo hali
EmoticonEmoticon