Prof. Muhongo aamuru
kukamatwa mitambo ya
Mwekezaji
Jan 16th, 2016 · 0 Comment
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo, ameagiza kukamatwa
kwa mitambo na mali zote za Mwekezaji
katika Mgodi wa Makaa ya Mawe kwenye
msitu wa Kabulo wilayani Kyela mkoani
Mbeya kampuni ya Off-Route Technologies
ya Afrika Kusini kwa kosa la kuchimba
madini bila ya kuwa na leseni ya uchimbaji.
Waziri Profesa Muhongo, amesema licha ya
kampuni hiyo kuchimba madini na kuyauza
nje ya nchi bila ya kuwa na leseni pia hailipi
kodi za Serikali jambo linalolitia hasara
Taifa hivyo ameamuru kukamatwa kwa
mitambo hiyo ili kulinda maslahi ya Serikali.
Waziri Profesa Muhongo, ametoa agizo hilo
baada ya kuutembelea mradi wa uchimbaji
wa makaa ya mawe unaoendeshwa na
kampuni hiyo ya Off-Route Technologies ya
Afrika Kusini kwenye msitu wa Kabulo
wilayani Kyela mkoani hapa na kuelezwa
kuwa kampuni hiyo inafanya shughuli hizo
bila ya kuwa na leseni ya uchimbaji wa
madini.
Imeelezwa kuwa baada ya Off-Route
Technologies kuamriwa na Baraza la Taifa
la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira,
NEMC, kusimamisha shughuli zake Oktoba
Mwaka 2014 kutokana na kukiuka masharti
ya mazingira, kampuni hiyo ilikimbilia
wilayani Chunya na kufanya shughuli za
uchimbaji bila ya kuwa na leseni hatua
ambayo sasa imeikera Serikali.
Utekelezaji wa agizo hilo upo mikononi mwa
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro,
ambaye amewaagiza Wakuu wa Polisi
katika wilaya za Kyela na Chunya kuchukua
hatua hizo.
Imebainishwa kuwa tangu Oktoba 2013
kampuni hiyo imekuwa hailipi Mrabaha kwa
madini inayoyauza ndani ya nchi bali
imekuwa ikilipa mrabaha kwa madini
inayoyauza nje ya nchi kwa sababu
inalazimika kufanya hivyo ili kupata kibali
cha usafirishaji wa madini hayo.
Meneja Biashara wa Off-Route
Technologies, Andrew Mark, amekanusha
tuhuma hizo na Serikali inatarajia kukutana
na uongozi wa kampuni hiyo Januari 18 ili
kushughulikia kasoro hizo.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon